Pata taarifa kuu
SOKA-UINGEREZA

Kocha wa Uingereza achunguzwa kwa madai ya kukiuka sheria za FA

Shirikisho la soka nchini Uingereza linachunguza sakata la kocha wa timu ya taifa Sam Allardyce kuhusika katika  usajili wa wachezaji kinyume na utaratibu wa Shrikisho hilo.

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uingereza  Sam Allardyce
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uingereza Sam Allardyce independent.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la The Telegraph limedai kuwa lina ushahidi kuwa kocha huyo aliingia kwenye mkataba wa Pauni za Uingereza 400,000 kufanya kazi hiyo kwa niaba ya Mawakala wa soka kutoka Mashariki ya mbali.

Inadaiwa kuwa mwaka 2014, kocha huyo akiwa na wakala wake na mshauri wake wa kifedha, alifanikisha usajili wa mchezaji Enner Valencia raia wa Ecuador kuichezea klabu ya West Ham  nchini Uingereza kutoka klabu ya Pachuca kutoka Mexico kwa kima cha Pauni Milioni 12.

Licha ya tuhma hizi, kocha huyo hajajitokeza kuzizungumzia. Viongozi wa soka nchini humo wamelitaka  Gazeti hilo kuwasilisha ushahidi huo ili wajiridhishe.

Shirikisho la soka nchini Uingereza lilipiga marufuku mchakato wa wachezaji kusalijiwa au kununuliwa  kupitia makocha au mtu mwingine  mwaka 2008.

Madai haya yanampata kocha Allardyce anayefahamika kwa jina maarufu la Big Sam baada ya kupewa kibarua cha kuifunza Uingereza mwezi Julai, baada ya kufutwa kazi kwa kocha wa zamani Roy Hodgson.

Ikiwa madai haya yatabainika kuwa kweli, basi kazi ya kocha huyu itakuwa hatarini wakati huu akijindaa kukitaja kikosi chake cha kwanza kitakachomenyana na Slovakia kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.