Pata taarifa kuu
ITALI-MICHEZO YA OLIMPIKI 2024

Roma yajiondoa kugombea kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki 2024

Meya mpya wa Roma, Virginia Raggi, ametangaza Jumatano hii, Septemba 21 kwamba asingeweza kuunga mkono kugombea kwa mji mkuu wa Italia kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki 2024, ikimaanisha kuondolewa kwa barua ya mji wa Roma katika kinyang'anyiro hiki.

Virginia Raggi, Meya wa Roma, avunja matumaini ya raia wa Italia ya kuandaa Michezo ya Olimpiki 2024.
Virginia Raggi, Meya wa Roma, avunja matumaini ya raia wa Italia ya kuandaa Michezo ya Olimpiki 2024. Andreas SOLARO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Virginia Raggi, aliyechaguliwa mwezi Juni 2016 katika uongozi wa manispaa ya mji wa Roma, alitangaza wakati wa kampeni yake kwamba kipaumbele cha mji si kuandaa Michezo ya Olimpiki. Kwa hiyo amtimiza ahadi yake.

"Ni ujinga kusema ndiyo kwa maombi haya. Hapana kwa Michezo ya kulazimishwa! Hapana kabisa! Hapana ujenzi wa kanisa katika jangwa, " Bi Raggi amesema katika mkutano na waandishi wa habari, baada ya zaidi ya miezi mitatuakiwa katika uongozi wa manispaa ya mji wa Roma.

"Hatutoweka rehani mustakabali wa mji huu," amesema, kabla ya kuongeza kuwa Michezo ya Olimpiki ni "aina ya ndoto inayobadilika kuwa kitu kisiyokuwa na mwelekeo kwa wakazi".

Itakubukwa pia kwamba meya ana vipaumbele vingine, kwa sababu ya madeni ya mji waRoma yanayokadiriwa kufikia Euro bilioni 13. Kwa hiyo, michezo hii ina uzito mkubwa kwa upande wa manispa ya mji, kwa sababu mji wa Rome haujamaliza kulipa mikopo inayohusiana na Michezo ya Olimpiki ya 1960.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.