Pata taarifa kuu
SOKA-CECAFA

Ethiopia kuanza kampeni ya kusaka taji la CECAFA dhidi ya Rwanda

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Ethiopia, inayofahamika kwa jina  la Lucy, inashuka dimbani kumenyana na She-Amavubi ya Rwanda katika mchuano wake wa kwanza hatua ya makundi kuwania taji la CECAFA kwa upande wa wanawake.

Timu ya taifa ya Kenya na Burundi zikichuana katika michuano ya kutafuta taji la CECAFA kwa upande wa wanawake nchini Uganda
Timu ya taifa ya Kenya na Burundi zikichuana katika michuano ya kutafuta taji la CECAFA kwa upande wa wanawake nchini Uganda Cecafa
Matangazo ya kibiashara

Michuano hii imeingia siku ya nne katika Taasisi ya mafunzo ya soka ya Njeru mjini Jinja nchini Uganda.

Huu ni mchuano wa pili wa Rwanda baada ya kufungwa na Kilimanjaro Queens ya Tanzania bara mwanzoni mwa wiki hii kwa mabao 3-2.

Rwanda inahitaji ushindi dhidi ya Ethiopia, kujihakikishia nafasi ya kucheza katika hatua ya nusu fainali.

Siku ya Jumanne, Harambee Starlets ya Kenya ilifuzu katika hatua ya nusu fainali baada ya kuishinda Burundi mabao 4-0, lakini pia kuilemea Uganda mabao 4-0 katika mchuano wa ufunguzi.

Uganda nayo iliishinda Zanzibar mabao 9-0 katika mchuano wake wa pili baada ya kupoteza mchuano wa ufunguzi dhidi ya Kenya.

Hadi sasa mabao 33 yamefungwa katika michuano hii ya CECAFA.

Ratiba ya siku ya Alhamisi Septemba 15 2016

  • Kenya vs Zanzibar
  • Uganda vs Burundi
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.