Pata taarifa kuu
UEFA-SOKA

Aleksander Ceferin achaguliwa kuwa rais wa UEFA

Aleksander Ceferin amechaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA), Jumatano hii, Septemba, akimrithi Michel Platini, raia wa Ufaransa.

Aleksander Ceferin (kulia) wakati wa mkutano mkuu wa UEFA, Jumatano Septemba 14 katika mji wa Athens.
Aleksander Ceferin (kulia) wakati wa mkutano mkuu wa UEFA, Jumatano Septemba 14 katika mji wa Athens. AP
Matangazo ya kibiashara

Ceferin, rais wa Shirikisho la Soka nchini slovenia, amechaguliwa kwa kura 42 katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) uliofanyika mjini Athens. Aleksander Cefirin amemshinda mshindani wake Michael van Praag kutoka Uholanzi.

Bw Cefirin, mwenye umri wa miaka 48 anamrithi mchezaji wa zamani wa kimataifa kutoka Ufaransa Michel Platini, ambaye alijiuzulu baada ya kusimamishwa mwaka jana na mahakama ya ndani ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Muhula wake utamalizika hadi mwaka 2019, muda uliyokua umebaki kwa Michel Platini kama rais wa UEFA.

"Ni heshima kubwa lakini pia jukumu kubwa," amesema Ceferin akizungumzia uchaguzi wake.

"Hii ina maana kubwa kwangu. Nchi yangu ndogo Slovenia imepata faraja na kutambuliwa zaidi duniani, na natumaini siku moja mtafurahia kazi yangu, " Cefirin ameongeza, akihutubia viongozi wa UEFA.

Aleksander Ceferin alisomea sheria na ni rais wa Shirikisho la Soka nchini Slovenia tangu mwaka 2011.

"Dhamiri yangu iko tulivu"

Mapema, Michel Platini alisema kuwa "dhamiri yake iko tulivu", katika hotuba yake ya kuaga mbele ya taasisi ya Soka barani Ulaya.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), limempa idhni ya kuzungumza kwa Kifaransa katika mkutano mjini Athens.

Michel Platini, mwenye umri wa miaka 61, alisimamishwa mwaka jana kushiriki shughuli zote zinazohusiana na soka kwa kukiuka sheria za maadili ya mchezo.

Anashtumiwa kunufaika mwaka 2011 na malipo yenye utata wa Euro milioni 1.8 kutoka kwa Joseph Blatter, rais wa FIFA aliyeondolewa madarakani kutokana na kashafa ya ufisadi katika taasisi hiyo ya kimataifa ya Soka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.