Pata taarifa kuu
SOKA-UEFA

Aleksander Ceferin achaguliwa kuwa rais mpya wa UEFA

Aleksander Ceferin, amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.

Rais mpya wa Shirikisho la soka barani Ulaya  Aleksander Ceferin
Rais mpya wa Shirikisho la soka barani Ulaya Aleksander Ceferin Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Ceferin mwenye umri wa miaka 48 ambaye ni wakili na raia wa Slovenia, alipata kura 42 na kumshinda rais wa Shirikisho la soka nchini Uholanzi Michael van Praag aliyepata kura 13.

Baada ya kuchaguliwa, Ceferin amesema wingu la mabadiliko sasa linavuma barani Ulaya.

Aidha, amesema anapoanza kazi hii mpya, anafahamu kuwa anatarajiwa kukabiliana na tuhma za ufisadi na tuhma za kuwepo kwa upangaji wa matokeo barani Ulaya.

“Nataka kuleta mambo mazuri, ambayo UEFA imekuwa ikifanya kwa sababu tumechoka na mambo yalivyo kwa sasa,” amewaambia wajumbe wa UEFA kutoka mataifa 55.

Ceferin, anachukua nafasi ya Mitchel Platini ambaye amepigwa marufuku na Shirikisho la soka duniani FIFA kwa madai ya ufisadi, baada ya kupokea Dola Milioni 2 kutoka kwa FIFA kwa kumshauri rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.