Pata taarifa kuu
SOKA-CECAFA

CECAFA: Kenya na Burundi kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali

Kenya na Burundi zinamenyana katika mchuano wa pili kuwania taji la CECAFA kwa upande wa wanawake, michuano inayoendelea nchini Uganda.

Timu ya taifa ya Tanzania bara na Rwanda wakimenyana Septemba 12 2016
Timu ya taifa ya Tanzania bara na Rwanda wakimenyana Septemba 12 2016 soka25east.com
Matangazo ya kibiashara

Mataifa haya mawili yanacheza mechi yao ya pili baada ya kushinda mechi za ufunguzi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mshindi kati ya Kenya na Burundi, atafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Mechi ya kwanza Kenya iliishinda wenyeji Uganda mabao 4-0, huku Burundi wakipata ushindi mkubwa wa mabao 10-1 dhidi ya Zanzibar.

Mchuano mwingine unaochezwa siku ya Jumanne, katika taasisi ya FUFA Njeru mjini Jinja ni kati ya wenyeji Uganda na Zanzibar.

Siku ya Jumatatu, Kilimanjaro Queens ya Tanzania bara iliishinda She-Amavubi ya Rwanda katika mchuano wa kundi B kwa mabao 3-2 .

Tanzania walianza vema kwa kupata mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza, mabao waliyofungwa na Asha Rashid na Stumai Abdalla.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye Rwanda ilirejea na kusawazisha mabao yote kupitia na Anne Marie na Anton Anastazia lakini baadaye Tanzania ikajipatia bao la ushindi katika dakika za lala salama.

 

Timu ya taifa ya Kenya ya wanawake, Harambee Starlets
Timu ya taifa ya Kenya ya wanawake, Harambee Starlets CECAFA

Ratiba
Jumatano Septemba 14 2016

  • Rwanda vs Ethiopia

Alhamisi Septemba 15 2016

  • Kenya vs Zanzibar
  • Uganda vs Burundi

Mechi za nusu fainali zitachezwa siku ya Jumamosi, Septemba tarehe 17 huku fainali ikipigwa siku ya Jumatatu tarehe 19.

Michuano hii inachezwa kwa mara ya pili kwa muda mrefu baada ya Zanzibar kuandaa michuano hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.