Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Serena atupwa nje US Open, kupoteza nafasi ya kwanza kwa Kerber

media Mchezaji Serena Williams akionekana mwenye huzuni mara baada ya mchezo wake dhidi ya Karolina Pliscova aliyemfunga na kutinga hatua ya fainali. Robert Deutsch-USA TODAY Sports

Mchezaji Karolina Pliskova raia wa Jamhuri ya Czech anayeshikilia nafasi ya 10 kwa ubora wa mchezo wa tenesi, amefanikiwa kumfunga Serena Williams na kutinga hatua ya fainali ya michuano ya US Open na kumaliza utawala wa mchezaji huyo kuwa nambari moja duniani.

Serena mwenye umri wa miaka 34 hivi sasa, alijikuta akifanya makosa ya kizembe yaliyosababisha ajikute akipoteza mchezo wake kwa matokeo ya seti 6-2, 7-6 na 7-5, matokeo ambayo sasa yanamfanya Pliskova kukutana na Mjerumani Angelique Kerber anayeshika nafasi ya pili kwenye mchezo wa fainali.

Matokeo haya pia yanamaanisha kuwa Kerber atashika nafasi ya kwanza kwa ubora wa mchezo huo upande wa wanawake baada ya kumalizika kwa michuano ya US Open akimpiku Serena.

Serena alikuwa akilenga kuwania taji lake la 23 la michuano mikubwa ya tenesi ili aweke rekodi, lakini akajikuta ndoto zake zikizimwa na Pliskova.

Mchezaji Karolina Pliskova akishangilia baada ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya US Open kwa kumfunga Serena Williams Robert Deutsch-USA TODAY Sports

Hata hivyo anaendelea kusalia na rekodi sawa na mchezaji tenesi mashuhuru Steffi Graf ambao wote wanashikilia rekodi moja ya kutwaa mataji makubwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja pamoja na taji la WTA kwa rekodi ya wiki 186 kuwa nambari moja duniani.

Akuzungumza mara baada ya mchezo wake, Serena amemsifu Pliskova, ambaye amesema alicheza vizuri na kukiri kuwa majeraha ya goti lake pia yalichangia kumfanya ashindwe kuwa kwenye kiwango bora.

Bingwa wa taji la Australian Open Mjerumani Angelique Kerber alimfunga Carolina Wozniacki raia wa Denmark kutinga hatua ya fainali kwa kumfunga kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-4 na 6-3.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana