Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGANDA-MCHEZO

AFCON 2017: Burkina Faso na Uganda wafuzu

Jumapili Septemba 4, 2016 timu za Burkina Faso na Uganda zimefuzu kwa hatua ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017. Uganda itacheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978, kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Comoro.

Mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Burkina, Faso Prejuce Nakoulma.
Mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Burkina, Faso Prejuce Nakoulma. BEN STANSALL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Burkina Faso, wenyewe, wameishia wa kwanza katika kundi hili la D baada ya ushindi dhidi ya Botswana (2-1).

Timu hizi mbili kutoka mataifa ya Burkina Faso na Uganda zimewashangaza wengi baada ya kujipatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili hii Septemba 4, 2016 itakayochezwa kuanzia tarehe 14 Januari hadi Februari 5 mwaka 2016 nchini Gabon.

Kama Waganda waliwabwaga Wacomoro kwa bao 1-0 kupitia mkwaju wa Farouk Miya, Burkina Faso, wao walisubiri mpaka dakika 99 za mchezo kubadili matokeo na kupata ushibdi dhidi ya Botswana.

Burkina Faso yaanza vizuri

Mashabiki wa Etalons, (timu ya taifa ya Burkina Faso) walikuwa kwa hakika wamekata tamaa, Jumapili hii mjini Ouagadougou.

Burkina Faso, ilianza vizuri kwa kupachika bao la kwanza, bao lililoingizwa na mchezaji Préjuce Nakoulma katika dakika ya 18. Mshambuliaji huyi alikosa fursa nyingi kuliona bao la Botswana. Lakini kufukuzwa kwa nahodha wa Botswana Lesego Galenamotlhale, ilipelekea wachezaji wa Paulo Duarte kuwa na matumaini ya kufanya vizuri.

Hata hivyo timu ya Botswana ilikuja juu, hadi dakika ya 44, ambapo ilisawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya Adama Guira kuunawa mpira katika eneo lake la hatari. Bao la kusawazisha la Botswana liliwekwa kimyani na Thabang Sesinyi.

Burkina Faso iliendelea kutawala mpiora dakika chache baada ya kufukuzwa kwa kipa wa Botswana, Kabelo Dambe, ambaye alipewa kwa mara ya pili kadi ya manjano katika dakika ya 87. Wakati huo huo mlinzi wa Burkina Faso, Steeve Yago, alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Lebogang Ditsele katika dakika ya 90 + 3.

Baada ya mkasa huo Burkina Faso ilicheza kwa kutumia nguvu nyingi, na dakika chache baadaye mchezaji wake Banu Diawara aliiokoa timu yake katika dakika ya 90 + 9 na hivyo kuipelekea kupata ushindi wa mabao 2 kwa 1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.