Pata taarifa kuu
TENESI

Serena, Venus na Murray wasonga mbele michuano ya US Open

Mchezaji tenesi Serena Williams, hakuonesha dalili zozote za kuwa anauguza majeraha ya bega na kushindwa kuendelea na mashindano ya US Open nchini Marekani, ambapo alifanikiwa kumfunga mpinzani wake Ekaterina Makarova, kwa seti mbili bila.

Mchezaji tenesi raia wa Mareakani,Serena Williams akishangilia baada ya kutinga mzunguko wa pili wa michuano ya US Open 2016
Mchezaji tenesi raia wa Mareakani,Serena Williams akishangilia baada ya kutinga mzunguko wa pili wa michuano ya US Open 2016 REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Serena ambaye anashikilia nambari moja kwa ubora wa mchezo wa tenesi upande wa wanawake, alionekana kusuasua katika seti ya kwanza dhidi ya Makarova, Mrusi anayeshikilia nafasi ya 29, ambapo alifanikiwa kumfunga kwa matokeo ya 6-3 na 6-3.

Akizungumza mara baada ya mchezo wake, Serena, aliwaambia wanahabari kuwa kwasasa anaendelea kufanya tathmini ya jeraha la bega alilonalo kabla ya kukabiliana na Vania King katika raundi ya pili ya michuano hiyo.

Dada yake Venus Williams anayeshikilia nafasi ya 6 kwa ubora wa mchezo huo, alifanikiwa kurekebisha makosa ya mapigo 63 na kumfunga Kateryna Kozlova wa Ukraine kwa matokeo ya seti 6-2, 5-7 na 6-4.

Mchezaji anayeshikilia nafasi ya 4 kwa ubora wa mchezo huo, Agnieszka Radwanska sambamba na mchezaji anayeshika nafasi ya tano Simona Halep walipoteza mchezo yao na kushindwa kusonga mbele.

Andy Murray
Andy Murray Reuters/Kevin Lamarque

Kwa upande wa wanaume wachezaji Stan Wawrinka, Kei Nishikori na Juan Martin del Porto walifanikiwa kusonga mbele.

Mchezaji nambari mbili kwa upande wa wanaume Andy Murray yeye alimfunga Lukas Rosol na kuwa Muingereza wa tano kufika hatua ya pili ya michuano ya mwaka huu ya US Open.

Murray alimfunga Rosol kwa seti 6-3, 6-2 na 6-2, na sasa atacheza na Muhispania Marcel Granollers.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.