Pata taarifa kuu
LIGI KUU UINGEREZA

Allardyce asema Hart atakuwemo kwenye kikosi chake kijacho

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce, anasema mlinda mlango wa klabu ya Manchester City, Joe Hart atakuwa kwenye kikosi chake kitakachocheza mchezo wa kufuzu kucheza kombe la dunia mwezo ujao dhidi ya Slovakia.

Kocha wa klabu ya Manchester City, Joe Hart akiwa kwenye mazoezi na klabu yake kabla ya mechi mwishoni mwa wiki
Kocha wa klabu ya Manchester City, Joe Hart akiwa kwenye mazoezi na klabu yake kabla ya mechi mwishoni mwa wiki Reuters / John Sibley Livepic
Matangazo ya kibiashara

Hart mwenye umri wa miaka 29, mpaka sasa haijaichezea klabu yake mchezo wowote msimu huu, na ameambiwa anaweza kuondoka ikiwa atapenda.

"Atakuwa kwenye kikosi changu, hilo halina ubishi, lakini kuhusu mustakabali wake huko mbeleni? siwezi kujua mpaka nizungumze nae." alisema Allardyce.

Jumapili ya wiki hii, kocha Allardyce anatarajiwa kutangaza kokosi cja wachezaji wake watakaelekea kwenye mchezo dhidi ya Slovakia, September 4 mwaka huu.

Hart ameichezea timu yake ya taifa mara 63, lakini alikuwa na wakati mbaya wakati wa mashindano ya kombe la Ulaya, yaliyofanyika nchini Ufaransa, ambapo alikuwa akifanya makosa yakizembe yaliyosababisha timu yake kutolea kwenye michuano hiyo.

Makosa makubwa aliyafanya kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya Wales na Iceland na kutupwa nje ya hatua ya 16 bora.

Hart amekuwa sio chaguo la kwanza la kocha Pep Guardiola, na sasa mlinda mlango wa Argentina, Willy Caballero ndio amekuwa chaguo la kwanza la kocha mpya wa klabu hiyo.

Klabu ya Everton imeonesha nia ya kutaka kumsajili mlinda mlango huyo ambaye ameonesha hana nia ya kutaka kujiunga na Sevilla wala Borussia Dortmund, klabu ambazo nazo zilionesha nia.

Mwishoni mwa juma klabu ya Barcelona ilitangaza kufikia makubaliano ya awali kuhusu usajili wa mlinda mlango wake Claudio Bravo anayetakiwa na Man City.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.