Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-SOKA

Brazil kumenyana na Ujerumani katika fainali ya Michezo ya Olimpiki

Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki Brazil, watavaana na Ujerumani siku ya Jumamosi katika fainali ya mchezo wa soka kutafuta medali ya dhahabu.

Wachezaji wa Brazil wakisherehekea ushindi dhidi ya Honduras mabao 6-0 Agosti 17 2016
Wachezaji wa Brazil wakisherehekea ushindi dhidi ya Honduras mabao 6-0 Agosti 17 2016 mirror.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Brazil ilifika katika hatua hiyo baada ya kuifunga Hondurus mabao 6 kwa 0 katika mchuano wa nusu uliopigwa jijini Rio de Janeiro Jumatano usiku.

Maelfu ya mashabiki wa soka nchini humo wanatarajiwa kufurika katika uwanja wa Maracana, kuwaunga mkono vijana wa nyumbani ambao mwaka 2014; wakati wa kombe la dunia walifungwa na Ujerumani mabao 7 kwa 1 na itakuwa fursa ya kipekee kulipiza kisasi.

Wachezaji wa Brazil wakisherehekea ushindi baada ya kufuzu katika hatua ya fainali Agosti 17 2016
Wachezaji wa Brazil wakisherehekea ushindi baada ya kufuzu katika hatua ya fainali Agosti 17 2016 mirror.co.uk

Nigeria ambayo ilishinda taji hili mwaka 1996, ililemewa na Ujerumani baada ya kufungwa mabao 2 kwa 0 mjini Sao Paulo.

Wawakilishi hao wa Afrika sasa watamenyana na Honduras kutafuta nafasi ya tatu siku ya Jumamosi mjini Belo Horizonte.

Wawakilishi wengine wa Afrika ambao walishiriki katika Michezo hii lakini wakaondolewa katika hatua ya makundi ni Algeria na Afrika Kusini.

Wachezaji wa Ujerumani wakisherehekea baada ya kufuzu katika hatua ya fainali
Wachezaji wa Ujerumani wakisherehekea baada ya kufuzu katika hatua ya fainali performgroup.com

Fainali kwa upande wa wanawake, itachezwa siku ya Ijumaa kati ya Sweden na Ujerumani huku wenyeji Brazil wakichuana na Canada kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu.

Wawakilishi wa Afrika kwa upande wa wanawake Afrika Kusini na Zimbabwe waliondolewa mapema katika hatua ya makundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.