Pata taarifa kuu
JUDO

Mchezaji wa Judo kutoka Misri arudishwa nyumbani

Mchezaji wa mchezo wea Judo Islam El Shehaby kutoka Misri amerejeshwa nyumbani kutoka katika Michezo inayoendelea ya Olimpiki, baada ya kukataa kumsalimu mpinzani wake Or Sasson kutoka Israel baada ya pambano lao kukamilika.

Islam El Shehaby (Kulia) akikataa kumsalimu mpinzani wake Or Sasson (Kushoto) baada ya pambano la Judo
Islam El Shehaby (Kulia) akikataa kumsalimu mpinzani wake Or Sasson (Kushoto) baada ya pambano la Judo telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Olimpiki IOC iliunga mkono hatua kwa kueleza kuwa inakwenda kinyume na taratibu za mchezo huo na michezo ya Olimpiki ya kumpaa mpinzani wako mkono kama ishara ya amani na urafiki.

Hatau ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, aliyepoteza pambano hilo katika mzunguko kwa kwanza, liliwakera viongozi wa Kamati ya Olimpiki ya Misri na kuamua kumrudisha nyumbani.

El Shehaby alizomewa na mashabiki wa mchezo huo baada ya kuondoka jukwani.

Ripoti zinasema kuelekea katika Michezo hii ya Olimpiki, kulikuwa na wanaharakati waliomtaka El Shehaby kujiondoa kwenye pambano hili kwa sababu alikuwa anakwenda kucheza na raia wa Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.