Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-SOKA

Michezo ya soka kuanza kurindima leo nchini Brazil

Michuano ya soka katika michezo ya Olimpiki inaanza leo nchini Brazil.

Uwanja wa soka wa Maraccana nchini Brazil
Uwanja wa soka wa Maraccana nchini Brazil Cntraveler.com
Matangazo ya kibiashara

Mechi za wanawake ndizo zinazofungua dimba katika uwanja wa Olimpiki wa Joa Havelange, mjini Rio de Janeiro.

Sweden itakuwa nchi ya kwanza kujitosa uwanjani kupambana na Afrika Kuisni, na baadaye wenyeji Brazil watachuana na warembo kutoka China.

Mechi zingine zinazochezwa leo kwa upande wa wanawake ni pamoja na Canada dhidi ya Australia na Zimbabwe itakayovaana na Ujerumani.

Marekani nao watakuwa katika uwanja wa Belo Horizonte kuchuana na New Zealand huku Ufaransa ikimenyana na Colombia.

Michuano ya ufunguzi kwa upande wa wanaume itachezwa kesho:-

  • Iraq vs Denmark
  • Brazil vs Afrika Kusini
  • Swden vs Colombia
  • Nigeria vs Japan
  • Fiji vs Korea Kusini
  • Mexico vs Ujerumani
  • Honduras vs Algeria
  • Ureno vs Argetina.

Mabingwa watetezi kwa upande wa wanaume ni Mexico huku kwa upande wa wanawake ikiwa ni Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.