Kerber na Serena kukutana fainali ya michuano ya Wimbledon
Bingwa mara sita, Mmarekani Serena Williams, amefanikiwa kutinga kwa mara ya tisa kucheza fainali ya michuano ya Tenesi ya Wimbledon, akiweka historia ya aina yake, na sasa atakutana na Mjerumani Angelique Kerber aliyemfunga dada yake, Venus Williams, aliyekuwa akilenga kuwa mchezaji mwanamke mkongwe kushinda taji hilo katika kipindi cha miaka 22.
Imechapishwa:
Serena ambaye anawania taji lake la saba la michuano ya Wimbledon na kulenga kupata taji lake kubwa la 22, ilimchukua dakika 48 pekee na sekunde 34, ikiwa ni nusu fainali ya kwanza iliyomalizika katika muda mfupi, baada ya kushinda kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-2 na 6-0 dhidi ya Elena Vesnina anayeshika nafasi ya 50.
Matumaini ya Serena kucheza fainali za mwaka huu dhidi ya dada yake kwa mara ya tano na mara ya tisa katika michuano mikubwa, yalizimwa wakati mchezaji nambari nne kwa ubora wa mchezo huo, Angelique Kerber, bingwa wa michuano ya Australian Open, kwa kumfunga kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-4 na 6-4.
Serena ambaye alikuwa anacheza mchezo wake wa 32 kwenye michuano mikubwa ya Tenesi, alimsambaratisha Vesnina na kisha kubusu uwanja mbele ya mwanamfalme wa Uingereza, Williams.
Fainali ya michuano hiyo sasa itamkutanisha Angelique Kerber na Serena Williams, ambao walicheza kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya US Open.