Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

[Diaporama] Wachezaji wa Iceland wapokelewa kama mashujaa

media Mashabiki wa timu ya taifa ya soka ya Iceland wakiingia mitaan katikati mwa mji, maandamano ambayo yalidumu nusu saa. Kisha wachezaji walielekea katika eneo ambako ilikua ikirushwa mechi kati ya Uingereza na Ufaransa. RFI/Alice Pozycki

Baada yakufungwa mabao 5-2 dhidi ya Ufaransa, timu ya taifa ya soka ya Iceland imeishia mbio zake katika hatua ya robo fainali katika michuano ya ombe la mataifa ya Ulaya (Euro 2016).

Timu hii iliporejea nyumbani, wachezaji walipokelewa na maelfu ya mashabiki ambao walikuja kuipongeza timu yao kwa fivijo na nderemo katika mji mkuu Reykjavik.

Mbele ya Hallgrimskirkja, kanisa kubwa lililojengwa kwa mfano wa roketi, mashabiki waliingia kutoka pande zote. Kwa miguu, kwa baiskeli au juu ya mabega ya wazazi wao, huku wakivalia nguo zenye rangi ya bendera ya taifa la Iceland.

Pamoja na kucheleweshwa kwa nusu saa kulingana na ratiba, lori lililokua limejaa askari polisi lilifika karibu na mashabiki. Na hivyo hali ndio ikazidi kuchukua sura nyingine, polisi iliomba umati wa watu kuondoka. Kila mtu alitii, licha ya kuwa na hamu ya kuona kikiwasili kikosi ambacho kilipelekea nchi kupata sifa nyingi katika kipindi hiki cha wiki tatu.

Kila mtu alitamani kuwaona wachezaji mbalimbali wa kikosi cha timu ya taifa ya Iceland katika mji mkuu wa nchi hiyo. Furaha mpaka sasa inaendelea nchini humo, licha ya kubanduliwa katika michuano hiyo. Baadhi ya raia wa Iceland wamesema timu ya taifa ya Iceland imejenga jina katika historia yake.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana