Pata taarifa kuu
ARGENTINA-LIONEL MESSI-SOKA

Soka: Maradona na Macri wamuomba Messi kufuta uamuzi wake

Rais wa Argentina Mauricio Macri na mchezaji wa zamani nyota nchini humo Diego Armando Maradona wamemtaka Lionel Messi kufuta uamuzi aliyochukua wa kustaafu na kuendelea kuichezea timu yake ya taifa. Rais Mauricio Macri pia amemtaka mchezaji huyo nyota kupuuzia kashfa zinazotolewa na wapinzani wake.

Lionel Messi achukua uamuzi wa kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina.
Lionel Messi achukua uamuzi wa kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina. REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

"Messi anapaswa kubaki katika timu ya taifa ya Argentina, anapaswa kubaki (...) Atakwenda Urusi kuwa bingwa wa dunia" katika michuano ya Kombe la Dunia 2018, Maradona amesema kwenye tovuti ya gazeti la kila siku la Argentina la NACION. Kwa upande wake, Rais wa Argentina amemtaka nyota wa soka duniani, Lionel Messi, na alimweleza kwamba "amekua akijisikia kuwa ni mwenye fahari akiwa katika timu ya taifa ya Argentina, na kumuuliza kutosikiliza maneno ya upuuzi yanayotolewa na wapinzani wake," msemaji wa serikali ameliambia shirika la habari la AFP. Lionel Messi, mwenye umri wa miaka 29 aliamua kustaafu kimataifa baada yatimu yake ya taifa kushindwa katika mechi dhidi ya Chile Jumapili ya wiki iliyopita katika michuano ya Copa America mwaka 2016.

Uamuzi wa Messi wa kustaafu kucheza soka la kimataifa, umewashangaza wengi, hasa ikiwa ni baada ya timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji la michuano ya Copa Amerika.

Mchezaji huyo na timu yake ya taifa kwa mara nyingine walishindwa kufua dafu katika ngazi ya kimataifa, ikiwa ni mara ya nne mfululizo kwa mchezaji huyu akiwa na timu yake ya taifa kushindwa kutwaa taji lolote kubwa baada ya siku ya Jumapili timu ya taifa ya Chile kuchomoza na ushindi kwa njia ya penalti. Chile iliingiza mikwaju minne, huku Argentina ikiingiza 2.

"Kwangu mimi, timu ya taifa nimemaliza," alisema Lionel Messi wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi na Chile.

"Nimefanya kila nilichoweza, nimeshiriki fainali nne, inauma kushindwa kuwa bingwa, ni wakati mgumu kwangu na timu nzima pia, na ni ngumu kusema, lakini nimemalizana na timu ya taifa ya Argentina," alisema Messi.

Uamuzi wa Messi uliwashangaza na bado unaendelea kuwashangaza wapenzi wa soka nchini Argentina na dunia kwa ujumla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.