Pata taarifa kuu
EURO 2016

Miamba itakayocheza hatua ya 16 bora yajulikana

Baada ya kumalizika kwa mechi za hatua ya makundi, hatimaye timu zitakazocheza kwenye hatua ya kumi na sita bora ya michuano ya kombe la Mataifa ya Ulaya 2016, zimejulikana.

Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya
Wafanyakazi wa Uefa wakitandaza uwanjani moja ya bango la shirikisho la mpira Ulaya REUTERS/Regis Duvignau Livepic
Matangazo ya kibiashara

Mechi za hatua ya kumi na sita bora zitaanza kuchezwa kwenye viwanja tofauti kuanzia Jumamosi ya tarehe 25 Juni.

Mechi zitakazopigwa siku ya Jumamosi, Juni 25, ni Uswisi watakao kuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Poland, kwenye mchezo ambao utachezwa kwenye mji wa Saint-Etienne, maajira ya saa kumi kamili za jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Wales ambao waliibuka vinara wa kundi lake, wao watakuwa jijini Paris, kucheza na timu ya taifa ya Ireland Kaskazini, mchezo ambao na wenyewe utapigwa Jumamosi, Juni 25, saa moja kamili kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezo wa mwisho kwa siku hiyo, utaikutanisha timu ya taifa ya Croatia watakaokuwa wakipepetana na timu ya taifa ya Ureno, ambayo iliponea kwenye tundu la sindano kutinga kwenye hatua hii baada ya kumaliza mchezo wake wa hatua ya makundi kwa sare ya mabao 3-3 na Hungary. Mechi itapigwa kwenye mji wa Lens.

Siku ya Jumapili, Juni 26, mechi za hatua ya 16 bora zitaendelea, ambapo mechi ya awali ya jioni, itakuwa ni kati ya timu ya taifa ya Ufaransa ambao ni wenyeji, watakaocheza na Jamhuri ya Ireland, mchezo ambao ni muhimu kwa wenyeji kushinda ikiwa wanataka kufika hatua ya fainali ya michuano ya mwaka huu kama wenyeji.

Mabingwa wa dunia, timu ya taifa ya Ujerumani, wenyewe watakuwa kwenye jiji la Lille, kucheza na timu ya taifa ya Slovakia, mchezo utakaoanza maajira ya saa moja kamili kwa saa za Afrika Mashariki.

Timu ya taifa ya Hungary, yenyewe itakuwa kwenye mji wa Toulouse, kucheza na timu ya taifa ya Ubelgiji, kwenye mchezo mwingine ambao wachambuzi wa mpira wanasema utakuwa wa kuvutia kutokana na viwango ambavyo timu hizi zimeonesha. Mechi hii itachezwa maajira ya saa nne kamili za usiku, saa za Afrika Mashariki.

Jumatatu, Juni 27, kutakuwa na mechi mbili tu za kukamilisha hatua ya 16 bora, ambapo mjini Saint-Denis, timu ya taifa ya Italia watakuwa na mtihani dhidi ya mabingwa mara mbili wa michuano hiyo, timu ya taifa ya Uhispania. Mechi hii itachezwa saa moja kamili za jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Jumatatu hiyohiyo ya Juni 27, timu ya taifa ya Uingereza yenyewe itakuwa ikipimana ubavu na timu ya taifa ya Iceland, kwenye mchezo ambao utachezwa kwenye mji wa Nice, maajira ya saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya kwa mwaka huu, mechi zake zitachezwa kuwanzia Alhamisi ya Junik 30m kwenye viwanja vinne tofauti.

Mechi ya kwanza itakuwa ni kati ya mshindi wa:

Mechi ya 1: Mshindi kati ya Uswisi au Poland atacheza na Mshindi kati ya Croatia au Ureno – Alhamisi, Juni 30.

Mechi ya 2: Mshindi kati ya Wales au Ireland Kaskazini atacheza na Mshindi katik ya Hungary au Ubelgiji – Ijumaa, July 1.

Mechi ya 3: Mshindi kati ya Ujerumani au Slovakia atacheza na Mshindi katik ya Italia au Uhispania – Jumamosi, July 2.

Mechi ya 4: Mshindi kati ya Ufaransa au Jamhuri ya Ireland atacheza na Mshindi kati ya Uingereza au Iceland – Jumapili, July 3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.