Pata taarifa kuu
LIGI KUU UINGEREZA

Everton yamtangaza Koeman kuwa kocha mkuu mpya

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza, hatimaye imemtangaza aliyekuwa kocha wa klabu ya Southampton, Ronald Koeman, kuwa kocha wake mkuu mpya, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kocha mkuu mpya wa Everton, Ronald Koeman
Kocha mkuu mpya wa Everton, Ronald Koeman Reuters / Paul Childs Livepic
Matangazo ya kibiashara

Kwa mantiki hiyo uongozi wa klabu wa Everton sasa utalazimika kulipa kiasi cha paundi za Uingereza milioni 5, ikiwa ni fidia kwa klabu ya Southampton kutokana na kuvunja mkataba wao na kocha huyo.

Koeman amekinia kikosi cha Southampton kwa muda wa miaka miwili.

Klabu ya Everton imekuwa bila ya kocha mkuu wa timu toka pale ilipotangaza kumfuta kazi kocha wake, Roberto Martinez, siku chache kabla ya kufungwa kwa pazia la ligi kuu ya Uingereza, msimu wa mwaka 2015/16.

Ronald Koeman aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Southampton.
Ronald Koeman aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Southampton. Reuters/Phil Noble

Muda mfupi baada ya kutangazwa kama kocha mkuu wa timu hiyo, Koeman amesema kuwa Everton ni mionongoni mwa vilabu vyenye historia nzuri na matarajio makubwa, na hivyo anatarajia kuifikisha mbali.

Mwenyekiti wa klabu wa Everton kwa upande wake akimtambulisha Koeman, amesema kuwa baada tu ya kuachana na kocha wao, Martinez, Mholanzi, Ronald Koeman alikuwa chagua lake la kwanza.

Mkataba kati ya Koeman mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, unaripotiwa kuwa na thamani ya paundi za Uingereza milioni 6 kwa mwaka, na alifikia makubaliano na klabu hiyo katikati ya wiki iliyopita.

Klabu ya Southampton ilimaliza kwenye nafasi ya sita chini ya kocha Koeman, ikiwa ni hatua kubwa kuwahi kufikiwa na klabu hiyo kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Koeman anatarajiwa kujiunga pamoja na kaka yake, Erwin na kocha wa viungo, Jan Kluitenberg, licha ya kuwa mkataba wao bado haujakamilika.

Everton pia ilikuwa inamwinda kocha mkuu wa Sevilla Unai Emery aliyetangaza kuachana na mabingwa hao wa kombe la Europa, pamoja na aliyekuwa kocha wa Manchester City, Manuel Pelegrini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.