Pata taarifa kuu
ROLAND GAROS

Muguruza amfunga Serena kushinda taji la French Open 2016

Muhispania, Garbine Muguruza amefanikiwa kumfunga bingwa nambari moja wa mchezo wa Tenesi, Serena Williams kwa seti mbili bila na kumuwezesha kushinda taji lake la kwanza kubwa la michuano ya French Open.

Garbiñe Muguruza akishangilia baada ya kushinda taji la French Open kwa mwaka 2016
Garbiñe Muguruza akishangilia baada ya kushinda taji la French Open kwa mwaka 2016 Fotos: Reuters
Matangazo ya kibiashara

Muguruza ambaye anashikilia nafasi ya nne kwenye orodha ya wachezaji Tenesi wanawake, alishinda fainali ya hii lei kwa seti 7-5 na 6-4 akilipiza kisasi cha kushindwa kushinda taji hilo kwenye fainali za mwaka jana.

Ushindi wa Muguruza mwenye umri wa miaka 22 hivi sasa, unakuwa ni ushindi wa kwanza kwa mchezaji Tenesi mwanamke raia wa Uhispania kushinda taji hilo la French Open tangu alipofanya mchezaji Arantxa Sanchez-Vicario mwaka 1998.

Serena Wiliams
Serena Wiliams REUTERS/Benoit Tessier

Serena mwenye umri wa miaka 34 hivi sasa, alikuwa ana matumaini ya kufanya vema kwenye fainali hii ili aweze kushinda taji lake la 22 la Grand Slams, ambalo lingemfanya ashikilie rekodi sawa na Steffi Grafs.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa fainali yao, Muguruza alisema kuwa amefurahi kucheza mchezo wa fainali na miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa bora zaidi duniani kwenye mchezo wa Tenesi. 

Muguruza akaongeza kuwa alilazimika kuwa makini kwa muda wote wa mchezo ili kuhakikusha analinda alama alizozipata dhidi ya Serena.

Serena ambaye kabla ya kuanza kwa michuano ya mwaka huu alielezwa kuwa majeruhi, amefanikiwa kufika fainali ya michuano ya mwaka huu kwa kishinda baada ya kuwafunga miongoni mwa wachezaji bora wa kike hadi kufikia kucheza na Mguruza.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.