Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-AFRIKA

CAF yaweka wazi hatua ya makundi

Hatimaye Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limeweka bayana hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho mwaka huu wa 2016.

Sierra Leone  dhidi ya Côte d'Ivoire, CAN 2015, mwezi Novemba 2014.
Sierra Leone dhidi ya Côte d'Ivoire, CAN 2015, mwezi Novemba 2014. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Mechi katika hatua hii zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi wa kwanza na wa pili watafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Kuna makundi mawili, kila kundi na vilabu vinne kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

Hata hivyo, ilikuwa ni pigo kubwa kwa klabu ya AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyoondolewa katika michuano ya klabu bingwa baada ya kubainika kuwa mchezaji wake Idrissa Traore aliichezea klabu yake hata baada ya kupigwa marufu ya mechi nne wakati akiichezea klabu ya Stade Malien ya Mali.

Nafasi yake imechukuliwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Michuano ya Klabu bingwa:

Kundi A

  • Zesco United-Zambia
  • Al-Ahly-Misri
  • ASEC Mimosas-Cote Dvoire
  • Wydad Casablanca-Morroco

Kundi B

  • Enyimba-Nigeria
  • Zamalek-Misri
  • Es Setif-Algeria
  • Mamelodi Sundowns-Afrika Kusini.

Michuano ya kwanza itachezwa tarehe 17 mwezi Juni.

Michuano ya Shirikisho CAF:

Kundi A

  • MO Bejaia-Algeria
  • Young Africans-Tanzania
  • TP Mazembe-DRC
  • Medeama-Ghana

Kundi B

  • Kawkab Marrakech-Morroco
  • Etoile du Sahel-Tunisia
  • FUS Rabat-Morroco
  • Al-Ahli Tripoli-Libya.

Michuano ya kwanza itachezwa tarehe 17 mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.