Pata taarifa kuu
Kenya-Raga

Kenya yashinda taji la dunia la raga la Sevens series

Kenya imeandikisha historia katika mchezo wa raga kwa wachezaji saba kila upande baada ya kunyakua taji la dunia la Singapore ruby Sevens series.

Wachezaji wa Kenya wakisherehekea ushindi
Wachezaji wa Kenya wakisherehekea ushindi
Matangazo ya kibiashara

Timu hiyo inayofahamika kwa jina maarufu la Shujaa, iliishinda Fiji kwa alama 30 kwa 7 katika fainali iliyochezwa katika uwanja wa taifa na kushuhudiwa na mashabiki 45,000.

Mchezaji Collins Injera ametajwa mchezaji bora wa fainali kwa kuipa timu yake alama 20 na kufunga penalti ya ushindi.

Hii ni mara ya kwanza Kenya inayofunzwa na mchezaji wa zamani Benjamin Ayimba kushinda taji hili la dunia baada ya kufika fainali mara mbili mwaka 2009 nchini Australia na mwaka 2013 nchini New Zealand.

Kenya inajiunga na Afrika Kusini kuwa nchi ya pili barani Afrika kuwahi kushinda taji hili.

Kuelekea katika hatua ya fainali, Kenya iliishinda timu ya Ufaransa kwa alama 28 kwa 7 na baadaye Argetina alama 15 kwa 12.

Rais Uhuru Kenyatta kupitia ukurasa wake wa Twitter ameipongeza timu hiyo na kusema wameiletea Kenya sifa.

Miongoni mwa wchezaji wa kikosi hicho ni pamoja na Andrew Amonde, Collins Injera, Oscar Ayodi, Samuel Oliech, Nelson Oyoo ,Frank Wanyama, Humfrey Kayange miongoni mwa wengine.

Nafasi ya tatu imechukuliwa na Afrika Kusini ambayo iliishinda Argetina kwa alama 28 kwa 0.

Mashindano yajayo yatafanyika jijini Paris nchini Ufransa kati ya tarehe 13 hadi 15 mwezi ujao wa Mei huku mashindano ya mwisho yakifanyika jijini London nchini Uingereza baadaye mwezi ujao.

Mataifa 15 hushiriki katika mashindano haya ya World rugby sevens series ni pamoja na,Argentina , Australia , Canada, Uingereza , Fiji ,Ufaransa ,Kenya ,New Zealand, Ureno ,Urusi ,Samoa ,Scotland ,Afrika Kusini na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.