Pata taarifa kuu
KENYA-SUDAN-SOKA

Kenya yalaumiwa kuchezesha wachezaji wasiostahili

Shirikisho la soka nchini Sudan linadai kuwa timu ya taifa ya soka ya Kenya yenye vijana wasiozidi umri wa miaka 20, ilikuwa na wachezaji watano waliokuwa zaidi ya umri huo.

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Kenya na Sudan kutoka sare ya bao 1 kwa 1 siku ya Jumapili wiki iliyopita jijini Khartoum, katika mchuano muhimu wa kusaka nafasi ya kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa itakayofanyika nchini Zambia mwaka ujao.

Mwekahazina wa Shirikisho hilo Oussama Ataelmaan, amesema kuwa Sudan itapeleka malalamisho yake kwa uongozi wa soka barani Afrika CAF.

Kanuni za CAF zinaweka wazi kuwa, ni wachezaji waliozaliwa baada January mwaka 1997 na baadaye ndio wanaoruhusiwa kushiriki katika mashidano hayo.

Sudan inasema kuwa wachezaji hao wa Kenya walizaliwa mwaka 1996.

Hata hivyo, rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Nick Mwendwa ametupilia mbali madai hayo na kusema wachezaji wote walichunguzwa kwa makini kabla ya mchuano huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kenya kujikiuta katika hali hii, mwaka 2003, CAF iliipiga marufuku Kenya kutoshiriki katika michuano ya vijana wasiozidi miaka 17 baada ya kubainika kuwa kulikuwa na wachezaji waliokuwa na umri mkubwa wakati huo na kuishinda Ghana mabao 3 kwa 2.

Mwaka 2014, Gambia ilifungiwa na CAF kwa miaka miwili kwa kosa hilo la kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa katika timu yake ya timu ya vijana wasiozidi miaka 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.