Pata taarifa kuu
REAL MADRID-AS ROMA-UEFA

Ligi ya Mabingwa: Real Madrid yaiyadhibu AS Roma

Klabu ya Real Madrid ikiwa ugenini imeiyadhibu AS Roma kwa mabao 2-0 katika mechi ya awali ya mzunguko wa nane ya Jumatato hii usiku katika michuano ya ligi ya Mabingwa ya UEFA, licha ya kutoonyosha mchezo mzuri.

Cristiano Ronaldo akikimbia hadi mikononi ya kocha wake Zinedine Zidane baada ya kufungua bao dhidi ya Roma. Februari 17, 2016.
Cristiano Ronaldo akikimbia hadi mikononi ya kocha wake Zinedine Zidane baada ya kufungua bao dhidi ya Roma. Februari 17, 2016. AFP PHOTO / ALBERTO PIZZOLI
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa real Madrid ina matumaini ya kufanya vizuri katika uwanja wake katika mchuano wa marudiano. Zinedine Zidane ameanza kujizoela sifa baada ya klabu yake kuanza kufanya vizuri.

Katika uwanja wa AS Roma, Zinedine Zidane alikua amekata tamaa akiwa ugenini licha ya klabu yake kupata ushindi huo muhimu. Klabu hii imeshindwa mchezo kwa muda wa karibu saa nzima ya mchezo, na hali hiyo ndio ilikua ilimkatisha tamaa Zidane.

Kipindi cha kwanza kimemalizika timu zote mbili zikiwa sare ya kutofungana. Lakini katika kipindi cha pili Real Madrid kupitia wachezaji nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo na Jese ilionyesha ubingwa wake.

Bao la kwanza la Real Madrid limewekwa kimyani na Cristiano Ronaldo katika dakika ya 57.

Real Madridi ilikuja juu baada ya mchezaji Jese kuingia uwanjani na kufanikia kupachika bao la pili katika dakika ya 86.

"Ushindi unanifanya kuwa na furaha kubwa. Hasa kwa timu ambayo ilituweka katika matatizo," alisema Zinedine Zidane mechi ilipomalizika.

Pamoja na ushindi huo, Real ina 100% ya bahati ya kufuzu katika robo fainali ya mechi ya marudiano kulingana na takwimu kutoka shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA. Ni hatua rahisi kwa timu iliyovunja rekodi kwa kutunukiwa tuzo mara kadhaa katika Ligi ya Mabingwa na kwa Zidane ambaye tayari alishinda mara mbili kama mchezaji (2002) na kocha msaidizi (2014).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.