Pata taarifa kuu
PSG-CHELSEA-UEFA-SOKA

Ligi ya UEFA: PSG yaibwaga Chelsea

PSG wamewapiga Chelsea (2-1) Jumanne hii, Februari 16, 2016, katika mechi ya nguvu kubwa wakati wa mzunguko wa nane wa mechi ya awali iliyochezwa katika uwanja wa Parc des Princes. Mchezaji wa Chelsea kutoka Nigeria, Obi Mikel, alifunga bao la matumaini kwa mechi ya marudiano katika wiki tatu.

Edison Cavani, raia wa Uruguay amefunga na kuipa matumaini PSG dhidi ya Chelsea Februari 16, 2016.
Edison Cavani, raia wa Uruguay amefunga na kuipa matumaini PSG dhidi ya Chelsea Februari 16, 2016. Reuters / Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Benfica wameiburuza Zenit St-Petersburg katika mechi ya mkondo wa kwanza ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.

PSG ikiwa nyumbani imetamba uwanjani dhidi ya Chelsea ambayo ina matumaini ya kufanya vizuri katika mechi ya marudiano.

Paris St-Germain walianza kuonyesha ushujaa wao baada ya kiungo wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic, raia wa Sweden kupachika bao la kwanza katika dakika ya 39.

Chelsea walisawazisha katika dakika ya 45 kupitia kwa mchezaji Mikel Obi, raia wa Nigeria, kabla ya Edison Cavan kufunga bao la pili katika dakika ya 78, na hivyo hadi kipenga cha mwisho Chelsea walijikuta wameburuzwa mabao 2-1.

Kwa upande mwengine Benfica wakichezea nyumbani waliwacharaza Zenit St-Petersburg kwa kuwafunga bao 1-0. Bao ambalo lilifungwa na Jonas muda wa ziada kutokana na mkwaju wa adhabu uliopigwa na Nicolas Gaitan.

Zenit walisalia wachezaji kumi uwanjani baada ya Domenico Criscito kupewa kadi ya pili ya njano katika dakika ya 90.

Siku ya Jumatano, Real Madrid ya Zinedine Zidane itajielekeza kwenye uwanja wa AS Roma, wakati ambapo AA Gent watawapokea Wolfsburg.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.