Pata taarifa kuu
CHAN 2016-DRC-CAMEROON

CHAN 2016: Cameroon yaiburuza DRC na zote zafuzu robo fainali

Rwanda-DRC na Cameroon-Côte d’Ivoire zitakutana katika robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika, Januari 30. Cameroon hatimaye imechukua nafasi ya kwanza katika Kundi B kutokana na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya DRC, Jumatatu hii Januari 25 katika uwanja wa mpira wa Huye, nchini Rwanda.

Wachezaji wa Cameroon Frank Thierry Boya (kushoto) na Yazid Atouba.
Wachezaji wa Cameroon Frank Thierry Boya (kushoto) na Yazid Atouba. Courtesy of cafonline
Matangazo ya kibiashara

Florent Ibenge, kocha wa DRC, aliwaonya mapema wachezaji wake: mechi ya mwisho ya kundi B ya CHAN 2016 itatuomba tukaze vibwebwe. Onyo halikutosha. Chui wa DR Congo wameshindwa na kuwapa nafasi ya kwanza Cameroon, Jumatatu hii Januari 25 katika uwanja wa mpira wa Huye.

Yazid Atouba aipatishia njia Cameroon

Wachezaji wa Cameroon ambao wameonekana hatari tangu mwanzoni wa mchuano dhidi ya DRC, iliyoonekana kubadili baadhi ya wachezaji ikilinganishwa na mchezo wake dhidi ya Angola (4-2). Kutoka sekunde ya 20 tangu kuanza kwa mechi hii, mshambuliaji Samuel Nlend alionekana peke yake dhidi ya Matampi Ley, kipa wa Leopards, lakini alishindwa na kupiga mpira nje. Katika nusu saa ya mchezo, Samuel Nlend, alipewa mpira kutoka upande wa kati, lakini alijikuta akikabiliwa na Ley Matampi.

Simba wa Nyika mwengine hatari ni Yazid Atouba. Kiungo huyo alionyesha katika mchezo huu kuwa hana mpinzani. Katika dakika ya 40, aliipatishia timu yake bao la kwanza, baada ya kupewa pasi, na hivyo kupelekea Cameroon kuandikisha bao 1-0.

Majibu mafupi kwa DRC

Muda mfupi baada ya mapumziko, Florent Ibenge, kocha wa Chui wa DRC, alibadili baadhi ya wachezaji na kuiimarisha safa ya nyuma na kati ya timu yake kwa kumuingiza beki Junior Baometu na kiungo wa kati Elia Mechak. Katika dakika ya 47, mshambuliaji wa DRC Jean-Marc Makusu aliipatishia timu yake bao la kusawazisha na hivyo matokea kubadilika: 1-1.

Hata hivyo Cameroon hawakukatika nguvu, walikuja juu, na katika dakika ya 52, Brice Moumi aliingiza bao la pili: 2-1, 52.

Bao la tatu la Cameroon lilifungwa katika dakika ya 64 na mchezaji Samuel Nlend: 3-1.

Kwa ushindi huo, Cameroon itabaki mjini Huye ambapo watakuwa na mechi na Côte d’Ivoire Januari 30, katika mchuano wa robo fainali ya CHAN 2016. DRC wenyewe, watamenyana na Rwanda siku hiyo hiyo mjini Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.