Pata taarifa kuu
EL Salvador-MAUAJI-SOKA

Alfredo Pacheco auawa kwa kupigwa risasi

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya El Salvador Alfredo Pacheco ameuawa kwa kupigwa risasi, katika kituo cha mafuta katika mji wa Santa Ana, kilomita 76 magharibi mwa mji mkuu wa San Salvador, vyanzo vya usalam vimebaini.

Askari polisi wakitembea mbele ya mmoja wa watu waliouawa na kundi la majambazi katika mji wa San Pedro Perulapan, nchini El Salvador, katika sambulizi dhidi ya basi, Agosti 5, 2015.
Askari polisi wakitembea mbele ya mmoja wa watu waliouawa na kundi la majambazi katika mji wa San Pedro Perulapan, nchini El Salvador, katika sambulizi dhidi ya basi, Agosti 5, 2015. REUTERS/Jose Cabezas
Matangazo ya kibiashara

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 33, aliyechezea El Salvador mechi nyingi zaidi za kimataifa, alipigwa marufuku maisha baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mechi 2013.

Polisi wanasema watu wengine wawili walijeruhiwa kwenye shambulio hilo, ambalo polisi bado wanachunguza dhamira yake.

Pacheco na wachezaji wengine 13 walipatikana na hatia ya pokea hongo timu hiyo ishindwe mechi kadha kati ya 2010-13.

El Salvador, taifa ndogo lililoko Amerika ya Kati, ni moja ya mataifa yenye viwango vya juu zaidi vya mauaji.

Mapema mwezi huu, mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta, 26, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa likizoni katika mji wake wa kuzaliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.