Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
Michezo

Tanzania bara na Uganda Cranes zapata ushindi, Zanzibar yaanguka

media

Matumaini ya Zanzibar kufuzu katika hatua ya mwondoano ya michuano ya soka ya CECAFA baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yamedidimia baada ya kupoteza mchuano wake wa pili Jumanne jioni katika uwanja wa Kimataifa wa Awassa nchini Ethiopia.

Uganda Cranes ambayo ilipoteza mchuano wake wa kwanza dhidi ya Kenya, ilipata ushindi mkubwa wa mabao 4 kwa 0 dhidi ya Zanzibar Heros katika mchuano wa pili wa kundi B.

Kuelekea mchuano huu, kocha Milutin 'Micho' Sredojevic alifanya mabadiliko matatu baada ya kufungwa na Kenya mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa kwanza.

Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza, Uganda walikuwa wanaongoza kwa mabao 2 kwa 0 mabao yote yalitiwa kimyani na mshambuliaji matata Farouk Miya ambaye pia alifungwa kwa penalti.

Uganda ilitawala mchezo huo huku kipa wa Zanzibar Ali Mwadini akiondolewa uwanjani kwa kupewa kadi nyekudu kwa uchezaji mbaya.

Mashabiki wa Uagnda

Mabao mengine ya Uganda yalifungwa na Erisa Ssekisambu na Ceaser Okhuti katika dakika 78 ya mchuano huo.

Uganda wanaongoza kundi la B kwa alama tatu kwa sababu ya wingi wa mabao, inafuatwa na Kenya na Burundi ambazo zina alama tatu.

Zanzibar ambayo itacheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Kenya siku ya Ijumaa haina alama yoyote hadi sasa.

Mchuano mwingine uliochezwa mjini Awasa siku ya Jumanne ni kati ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania bara ambayo iliifunga Amavubi Stars ya Rwanda mabao 2 kwa 1.

Ushindi huu umeipa Tanzania matumai makubwa ya kufika katika hatua ya mwondoano na inaongoza kundi la A kwa alama sita.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stasr wakisherehekea ushindi

Rwanda ambayo ilipata ushindi katika mchuano wake wa kwanza dhidi ya wenyeji Ethiopia, ni wa pili kwa alama tatu huku Ethiopia ikiwa ya tatu na Somalia ya nne.

Siku ya Jumatano, Malawi itamenyana na Djibouti huku Sudan Kusini ikicheza na jirani yake Sudan.

Mchuano mwingine Somalia watamenyana na Ethiopia huku mabingwa watetezi Kenya wakimenyana na Burundi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana