Pata taarifa kuu
FIFA

Blatter na Platini hatarini kufungiwa miaka saba

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA aliyesimamishwa kazi Sepp Blatter na Naibu wake Michel Platini huenda wakafungiwa kushiriki katika maswala ya soka kwa muda wa miaka saba ikiwa watapatikana na makosa ya kuhusika na ufisadi.

Sepp Blatter na Mitchel Platini
Sepp Blatter na Mitchel Platini
Matangazo ya kibiashara

Ripoti inasema Kamati ya nidhamu ya FIFA huenda ikapendekeza adhabu hiyo baada ya ikiwa itabainika kuwa Blatter alitoa malipo yasiyokuwa rasmi kwa Platini yanayokadiriwa kuwa Dola Milioni 2.

Kamati hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wake mwezi ujao wa Desemba, na imewafungia wawili hao kutoshiriki kwa shughuli za soka kwa siku tisini.

Platini na Blatter wote kwa pamoja wameendelea kukanusha kuhusika na tuhma hizo za ufisadi, huku Platini ambaye pia ni rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya akisema malipo aliyopata yalikuwa ni baada ya kumshauri Blatter kuhusu maswala mbalimbali ya soka.

Jaji Hans Joachim Eckert kutoka Ujerumani anaongoza uchunbguzi dhidi ya wawili hao.

Katika hatua nyingine, Blatter amesema alikuwa anahofia kufariki dunia siku chache zilizopita alipolazwa hospitalini baada ya kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Blatter mwenye umri wa miaka 79 alisema, β€œ Nilikuwa katikati ya Malaika na shetani aliyekuwa anawasha moto lakini Malaika walikuwa wanaimba nyimbo,”.

β€œNilikaribia kufa.Wakati mwingine nilihisi mwili wangu umechoka na umefika mwisho,”. aliongeza Blatter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.