Pata taarifa kuu
CECAFA-SOKA

Michuano ya CECAFA yaanza Jumamosi wiki hii

Michuano ya soka ya timu za taifa kati ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inaanza leo Jumamosi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugambachajitupa uwanjani dhidi ya Zanziba katika ufunguzi wa michuano ya CECAFA, Addis Ababa..
Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugambachajitupa uwanjani dhidi ya Zanziba katika ufunguzi wa michuano ya CECAFA, Addis Ababa.. RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Burundi watafungua mashindano hayo ya kila mwaka kuanzia saa nane mchana saa za Afrika Mashariki dhidi ya Zanzibar huku wenyeji Ethiopia wakimenyana na Rwanda.

Mabingwa watetezi wa taji hili ni Harambee Stars ya Kenya ambao wataanza kutetea taji lao dhidi ya Uganda siku ya Jumapili.

Mchuano mwingine wa Jumapili utakuwa kati ya Somalia na Kilimanjaro Stars ya Tanzania.

Malawi imealikwa katika mashindano haya na itaanza michuano hii dhidi ya Sudan siku ya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.