Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-AFRIKA

Orlando Pirates na Etoile du Sahel zamenyana Jumamosi wiki hii

Fainali ya kwanza kuwania taji la Shirikisho barani Afrika itachezwa Jumamosi wiki hii kati ya klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mfungaji wa Etoile du Sahel, Emika Opara, akikabiliana na nahodha wa CSS, Issam Merdassi.
Mfungaji wa Etoile du Sahel, Emika Opara, akikabiliana na nahodha wa CSS, Issam Merdassi. (Photo : AFP/Fethi Belaid)
Matangazo ya kibiashara

Fainali hiyo ya kwanza itachezwa katika uwanja wa Orlando Stadium huku fainali ya pili ikichezwa tarehe 29 ugenini jijini Tunis.

Mabingwa watetezi Al Ahly walibanduliwa katika michuano hii ambapo vlabu kutoka Tunisia vimekuwa vikitamba kwa muda mrefu.

CS Sfaxien ndio klabu iliyofanikiwa sana katika mahsindano haya ya Shirikisho kwa kushinda mataji matatu.

Etoile du Sahel ilishinda taji hili mwaka 2006 na kumaliza wa pili mwaka 2008.

Hakuna klabu ya Afrika Kusini ambayo imewahi kushinda taji hili.

Mshindi wa taji hili mbali na kupata kombe atakabidhiwa pia Dola za Marekani Laki 625.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.