Pata taarifa kuu
TP MAZEMBE-USM ALGER-SOKA

Soka: Mazembe yatwaa taji la klabu bingwa

TP Mazembe imekua bingwa wa soka barani Afrika kwa mara ya tano katika historia yake. Klabu hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya USM Alger katika mchuano wa marudiano wa fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika, Jumapili Novemba 8, 2015 mjini Lubumbashi.

Aly Samatta (katikati), mchezaji wa TP Mazembe katika mchuano wa fainali ya klabu bingwa dhidi ya USM Alger.
Aly Samatta (katikati), mchezaji wa TP Mazembe katika mchuano wa fainali ya klabu bingwa dhidi ya USM Alger. AFP PHOTO / FAROUK BATICHE
Matangazo ya kibiashara

Katika mchuano wa awalii, TP Mazembe iliiburuza USM ya Alger kutoka Algeria mabao 2-1.

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia imejitosa katika uwanja wake wa nyumbani mjini Lumbumbashi.

Mazembe imecheza fainali hii ikiwa na matumaini ya kunyakua taji hili baada ya kupata ushindi wa mabao 2 kwa 1 katika fainali ya kwanza mwishoni mwa juma lililopita ugenini.

TP Mazembe mabli na kuwa bingwa wa Afrika, atawakilisha bara la Afrika katika michuano ya dunia baina ya vlabu itakayochezwa nchini Japan mwezi Desemba mwaka huu.

TP Mazembe imekua nafasi kubwa ya kushinda kutokana na rekodi nzuri ya kupata ushindi ugenini nchini Algeria.

Historia inaonesha kuwa kati ya mechi 77 ambazo TP Mazembe imecheza tangu ilipoanza kushiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 1965, imepoteza tu michuano mitatu.

Kocha wa Mazembe Mfaransa Patrice Carteron, anaamini kuwa kazi kubwa bado ipo mbele yake na awali aliwaambia wachezaji wake kufanya mashambulizi ili kupata bao la mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.