Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA

Mechi 10 zapigwa katika viwanja mbalimbali Afrika

Mataifa 10 ya Afrika yanashuka dimbani hivi leo kumenyana katika mzunguko wa kwanza kutafuta nafasi ya kufuzu katika mzunguko wa pili ili kucheza katika mashindano ya dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Mashabiki wa Taifa Stars wakati ilipokua ikifuana na Cote d'Ivoire  June 16 mwaka 2013.
Mashabiki wa Taifa Stars wakati ilipokua ikifuana na Cote d'Ivoire June 16 mwaka 2013. YouTube
Matangazo ya kibiashara

Taifa Stars ya Tanzania itakuwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa kumi jioni kumeyana na Malawi.

Tanzania wanawategemea sana washambuliaji wake wa Kimataifa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe nchini DRC.

Timu hizi mbili zimekutana mara 43 tangu mwaka 1974 katika historia yao ya soka na Tanzania imeshinda mara 8, Malawi wameshinda mara 14 na nchi hizo mbili zimetoka sare mara 21.

Mchuano huu ni muhimu pia kwa kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye ametia saini mkataba wa miaka miwili na Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kuifunza Taifa Stars.

Harambee Stars ya Kenya wapo ugenini kuchuna ana Mauritius , huku Burundi wakipambana na Ushelisheli.

Kenya watakuwa wanamtegemea sana kiungo wa Kati Victor Wanyama anayechezea

Klabu ya Southampton nchini Uingereza na mshambuliaji matata Michael Olunga anayechezea klabu ya Gor Mahia.

Hata hivyo, macho na masikio ni kwa Sudan Kusini ambayo inaandikisha historia kwa kushiriki katika michuano hii ya kufuzu katika fainai za kombe ka dunia kwa mara ya kwanza.

Vijana hao kutoka jiji la Juba watakuwa wenyeji wa Mauritania.

Comoros wanacheza na Lesotho na kwa mara ya kwanza Sudan Kusini inaweka historia kwa kuanza harakati za kufuzu kwenda Urusi na Jumatano hii itapambana na Mauritania.

Kesho Sao Tome itakuwa nyumbani kupambana na Ethiopia huku Liberiaq ikimenyana na Guine Bissau.

Mataifa haya yatarudiana baada ya wiki moja na mshindi kufuzu katika mzunguko wa pili.

Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda tayari yamefuzu katika mzunguko wa pili wa michuano hii.

Hatua ya tatu ya kufuzu itakuwa ya makundi, kutakuwa na makundi matano na mshindi wa kila kundi atafuzu katika michuanoa hiyo ya dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.