Pata taarifa kuu
KENYA-CHINA-MASHINDANO-RIADHA-MICHEZO

Kenya yavunja rekodi katika mashindano ya Riadha China

Imekuwa ni siku ya furaha kwa wanariadha wakenya katika mashindano ya dunia ya Riadha yanayoendelea jijini Beijing, nchini China.

Ezekiel Kemboi, ameweka historia kwa kuwa mwanaridha wa kwanza kwa kushinda mataji manne ya dunia katika mashindano ya dunia ya Riadha.
Ezekiel Kemboi, ameweka historia kwa kuwa mwanaridha wa kwanza kwa kushinda mataji manne ya dunia katika mashindano ya dunia ya Riadha. REUTERS/Dylan Martinez
Matangazo ya kibiashara

Katika mbio za Mita elfu tatu kuruka maji na viunzi kwa mara nyingine Ezekiel Kemboi ametetea taji lake la dunia kwa kumaliza wa kwanza na ameweka historia kwa kuwa mwanaridha wa kwanza kwa kushinda mataji manne ya dunia katika mbio hizi.

Kenya ilitawala mbio hizi huku Conseslus Kipruto akishinda nafasi ya pili, Brimin Kiprop Kipruto akichukua nafasi ya tatu na kushinda medali ya shaba huku nafasi ya nne ikimwendea mkenya mwingine Jairus Birech.

Katika mbio za Mita elfu 10 kwa upande wa wanawake, Vivian Cheruiyot pia raia wa Kenya alichukua nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mwiethiopia Gelete Burka na Mmarekani Emily Infeld akamaliza katika nafasi ya tatu.

Kenya kwa sasa inaongoza jedwali ya nchi bora katika mashindano haya ikiwa na medali 6, mbili za dhahabu, mbili za fedha na mbili za shaba.

Jamaica ni ya pili kwa medali tatu baada ya kushinda mita 100 kwa upande wa wanaume na wanawake.

Mashindano haya yanaendelea siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.