Pata taarifa kuu
PSG-DI MARIA-SOKA

Angel Di Maria, nyota mpya wa Paris Saint-Germain

Kila majira ya joto kwa muda wa miaka minne, PSG imevunja rekodi kwa kununua wachezaji nyota kwa kitita kikubwa cha pesa. Mwaka huu 2015 mchezaji nyota kutoka Argentina, Angel Di Maria, ndiye amechaguliwa kujiunga na klabu ya PSG.

Angel Di Maria ajiunga na klabu ya PSG.
Angel Di Maria ajiunga na klabu ya PSG. AFP PHOTO / YURI CORTEZ
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo wa kati wa Argentina aliombwa tangu mwaka jana kujiunga na klabu hiyo, na Alhamisi, Agosti 6, ameonyeshwa rasmi kuwa tayari amejiunga na PSG. Na anasubiriwa kushiriki michuano mbalimbali ya msimu huu.

Angel Di Maria, amenunuliwa kwa kitita cha euro milioni 63, na amesaini mkataba wa kuichezea PSG kwa kipindi cha miaka minne.

Kila msimu PSG yapata mchezaji nyota mpya

Tangu kuwasili kwa QSI (Qatar Sports Investments) katika uongozi wa klabu ya PSG miaka minne iliyopita, wachezaji kadhaa walinunuliwa kutoka vlabu vingine na kujiunga na klabu hii ya Ufaransa. Javier Pastore alinunuliwa (euro milioni 43) mwaka 2011, Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva walinunuliwa (zaidi ya milioni 60) mwaka 2012, Edinson Cavani alinunuliwa (milioni 64) mwaka 2013 na David Luiz alinunuliwa (milioni 50 mwaka 2014. Di Maria anaongeza idadi kwenye orodha hii ya wachezaji walionunuliwa kwa kitita kikubwa cha pesa.

Di Maria atacheza katika klabu moja na David Luiz

Mwaka uliopita Di Maria aliondoka Real Madrid baada ya kukataa kuongeza mkataba. Wasiwasi wake: alitaka kuendelea katika nafasi ya winga wa kulia. Aliondoka Merengue kwa michuano ya Ulaya. Angel Di Maria aliwasili barani Ulaya chini ya bendera ya klabu ya Benfica Lisbon. Katika klabu ya PSG,atakutana na MBrazil David Luiz, mchezani aliyenunuliwa kwa kitita kikubwa cha pesa msimu uliopita.

Angel Di Maria anakuja kuongezea nguvu kwa kikosi cha PSG, ambacho kimekua ni gumzo nchini Ufaransa kwa kunyakua tuzo mbalimbali. Msimu huu, PSG tayari imemnunua kipa wa Ujerumani Kevin Trapp kwa euro milioni 10 na kiungo Benjamin Stambouli kwa euro milioni 9.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.