Pata taarifa kuu
TENNIS-MCHEZO

Tennis: Andy Murray na Vasek Pospisil wachuana leo

Michuano ya Tennis ya Wimbledon inaedelea leo na ni siku ya michuano ya robo fainali kwa upande wa wanaume.

Andy Murray, raia wa Uingereza anajiandaa kumenyana na Vasek Pospisil.
Andy Murray, raia wa Uingereza anajiandaa kumenyana na Vasek Pospisil. Reuters/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Mchuano wa kwanza ni kati ya Andy Murray na Vasek Pospisil na baadaye bingwa mtetezi Novak Djokovich atamenyana na Marin Cilic.

Katika mchezo mwingine , Roger Federer anachuana na Gilles Simon, huku Stan Wawrinka akipambana na Richard Gasquet.

Roger Federer - Andy Murray kaika fainali Wimbledon 2012.
Roger Federer - Andy Murray kaika fainali Wimbledon 2012. DR

Kwa upande wa wanawake, Mmarekani Serena Williams alimshinda Victoria Azarenka kwa seti tatu za 3-6, 6-2, 6-3 na kufuzu katika hatua ya nusu fainali.

Serena naye anacheza leo Jumatano na Mrusi, Maria Sharapova katika mchuano wa nusu fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.