Pata taarifa kuu
SENEGAL-MALI-SOKA

Senegal na Mali zamenyana Jumamosi

Timu za taifa za soka za Senegal na Mali zitacheza Jumamosi hii kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya kombe la dunia baina ya wachezaji wasiozidi miaka 20 inayofikia tamati New Zealand.

Seydou Sy,golkipa wa timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 20.
Seydou Sy,golkipa wa timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 20. RFI / David Kalfa
Matangazo ya kibiashara

Vijana wa Senegal waliondolewa katika hatua ya nusu fainali na Brazil siku ya Jumatano baada ya kufungwa mabao 5 kwa 0 huku Serbia wakiwashinda Mali mabao 2 kwa 1.

Fainali pia itachezwa Jumamosi mwishoni mwa juma hili kati ya Brazil na Serbia.

Nigeria na Ghana pia zililiwakisha bara la Afrika katika michuano hii ya dunia baina ya vijana duniani na kuondolewa.

Bingwa wa mwaka 2013 Ufaransa, naye aliondolewa mapema na mwaka huo Ghana walimaliza katika nafasi ya tatu.

Michuano ijayo itafanyika nchini Korea Kusini mwaka 2017.

Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yalishindwa kufuzu katika michuano hii na kuyaachia mataifa ya Afrika Magharibi kutamba na kuonesha ushupavu wao wa kusakata kabumbu.

Wachambuzi wa soka wanasema soka la vijana ndilo linaloweza kusaidia mataifa ya Afrika kuendelea kufanya vizuri katika michuano ya mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.