Pata taarifa kuu
KENYA-SOKA

Harambee Stars yajiandaa katika mchuano na Ethiopia

Kocha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Bobby Williamson, amekitaja kikosi cha wachezaji wanaosakata soka nyumbani kuanza maandalizi ya mchuano wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Ethiopia kufuzu katika michuano ya CHAN itakayofanyika nchini Rwanda mwakani.

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube
Matangazo ya kibiashara

Harambee Stars itakuwa ugenini jijini Addis Ababa kumenyana katika mchuano huo wa kwanza kabla ya kurudiana jijini Nairobi mapema mwezi ujao.

Kikosi cha Williamson kimewajumuisha wachezaji walioachwa wakati wa mchuano wa kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika dhidi ya Congo Brazaville mwishoni mwa juma lililopita.

Wachezaji walioachwa na wameitwa ni pamoja na kiungo wa kati wa Gor Mahia Ali Hassan Abondo na mshambuliaji wa AFC Leopards Jacob Keli.

Kikosi kamili:

Makipa: Boniface Oluoch (Gor Mahia), Ian Otieno (Posta Rangers), Boniface Baraza (Posta Rangers),

Mabeki :  Edwin Wafula (AFC Leopards), Brian Birgen (Ulinzi Stars), Sammy Meja (Thika United), David Gateri  (Bandari), Aboud Omar (Unattached), Jackson Saleh (AFC Leopards), Musa Mohamed (Gor Mahia)

Kiungo wa Kati :  Ali Abondo (Gor Mahia), Kevin Kimani (Tusker), Collins Okoth (Gor Mahia), Humphrey Mieno (Tusker),  Anthony  Ndolo (Sofapaka),  Bernard Mang’oli , Timonah Wanyonyi  (AFC Leopards) Eric Johanna  (Mathare United)

Washambuliaji :  Michael Olunga (Gor Mahia), Jesse Were (Tusker), Peter Nzuki (Nakumatt) , Jacob Keli, Noah Wafula, (AFC Leopards)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.