Pata taarifa kuu
MOROCCO-CAF-SOKA

Uamzi wa CAF dhidi ya Morocco wafutwa na TAS

Mahakama ya Usuluhishi kwa mchezo (TAS), ambayo ni mahakama huru yenye makao yake makuu mjini Lausanne, imefuta vikwazo vilivyowekwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF dhidi ya Morocco.

Mehdi Benatia, mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco.
Mehdi Benatia, mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco. AFP PHOTO /FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo ulichukuliwa Alhamisi wiki hii, mjini Lausanne, Uswisi.

Morocco ilikataa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Afcon 2015 kwa tarehe ziliyopangwa, kwa hofu ya maambukizi ya Ebola. Mahakama hii imeiruhusu timu ya Morocco kushiriki katika kombe la Mataifa ya Afrika katika mwaka 2017 na 2019. Morocco ilikuwa ilitengwa katika michuano hiyo.

" Uamzi wa kusimamishwa kwa timu ya taifa ya Morocco kwa kutoshiriki katika awamu mbili za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika katika mwaka 2017 na 2019, umefutwa, na faini iliyotakiwa kulipwa na Shirikisho la Soka nchini Morocco imepunguzwa hadi dola 50,000 badala ya dola milioni moja”, imesema taarifa kutoka TAS.

Shirikisho la Soka la Morocco pia limeepuka faini nyingine ya Euro 8,000,000 iliyotakiwa kulipwa " kama fidia kutokana na uharibifu wa nyenzo endelevu iliyoupata Shirikisho la Soka barani Afrika CAF".

Itakumbukwa kwamba, Shirikisho la Soka la Morocco lilichukua uamazi wa kuifuta timu ya taifa ya Morocco kwenye orodha ya timu zitakazoshiriki michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Afcon katika mwaka 2017 na 2019, kwa sababu Morocco ilikataa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Afcon 2015 , michuano ambayo ilipangwa kuanza Januari 17 hadi Februari 8. Viongozi wa Morocco waliomba mara kadhaa kuahirishwa michuano hio kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya Ebola , ambavyo vilikua vikishuhudiwa Afrika Magharibi. CAF hatimaye iliamua kuhamishwa mashindano hayo katika nchi ya Equatorial Guinea. Côte d’Ivoire ndio iliyoibuka mshindi wa michuano hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.