Pata taarifa kuu
KENYA-MVUTANO-SOKA

Mvutano waendelea kati ya KPL na FKF

Kampuni ya ligi kuu ya soka nchini Kenya, KPL imekwenda Mahakamani jijini Nairobi kutaka kutupiliwa mbali kwa agizo la Mahakama linaloizuia kuendelea na ligi kuu ya soka nchini humo iliyoanza mwishono mwa juma lililopita.

Nairobi,mji mkuu wa Kenya.
Nairobi,mji mkuu wa Kenya. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la soka nchini humo FKF lilikwenda Mahakamani kuitaka Mahakama kusitisha ligi ya KPL inayoendelea kutoka na mvutano unaoshuhudiwa kati ya pande hizo mbili.

Hii inaamana kuwa ligi ya KPL imesitishwa hadi Mahakama itapotoa uamuzi na kesi hiyo itasikilizwa tarehe 3 mwezi ujao.

Kabla ya kwenda Mahakamani kumekuwa na ligi mbili nchini Kenya zikichezwa kwa wakati mmoja, ile ya KPL na ile ya Shirikisho la soka FK linaloongozwa na Sam Nyamweya.

Mvutano huo ulianza baada ya Shirikisho la soka nchini Kenya kutaka msimu huu kuwe na vlabu 18 lakini KPL ikakataa na kusema kutakuwa tu na vlkabu 16 kama ilivyo kawaida.

Hatua ya KPL iliikasirisha FKF ambayo ilisema haitambua ligi ya KPL na hivyo kupandisha vlabu vya daraja la chini katika ligi ya FKF.

Vlabu vilivyoshirki msimu uliopita, vimeamua kushiriki katika ligi ya KPL.

Wachambuzi wa soka nchini humo wanasema kuwa, ikiwa hali hii itaendelea itarudisha nyuma kiwango cha soka katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Shirikisho la soka duniani, FIFA liliandikia barua FKL na KPL kuzungumza ili kuafikiana lakini pande hizi mbili zimeshindwa kupata mwafaka.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kenya kuwa na ligi mbili kwa wakati mmoja, mwaka 2005 pia kulikuwa na sintofahamu kama hii na kusababisha kuvunjwa kwa Shirikisho la soka ili kutatua mzozo huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.