Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA / ULAYA

PSG na Chelsea zatoka sare ya 1-1

Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, zimeanza katika hatua ya kumi na sita bora, ambapo sare zilitawala katika mchuano wa ufunguzi Jumapili Februari 17.

Mchezaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic akijiuliza iwapo kwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea ni matokeo mazuri kwa timu yake.
Mchezaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic akijiuliza iwapo kwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea ni matokeo mazuri kwa timu yake. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Paris Saint Germain ya Ufaransa ikiwa nyumbani imejipima nguvu na Chelsea ya Uingereza, hadi dakika tyisini ya mchezo timu hizi mbili zikwenda sare ya kufungana bao 1-1.

Chelsea ndio walioanza kuliona lango la paris Saint Germain katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza, bao ambalo limefungwa na Branislav Ivanovic. Hadi dakika 45 ya kipindi cha kwanza cha mchezo Chelsea ilikua ikiongoza kwa bao 1-0

PSG hawakuta tamaa baada ya kupachiwa bao hilo. Wachezaji wa PSG waliendelea kulisakama lango la Chelsea. David Luiz, ambaye ni kiungo wa PSG, aliwadhibiti wachezaji wa timu yake ya zamani ya Chelsea. Mshambuliaji Matuidi wa PSG alilishambilia lango la Chelsea na kumfanya golkipa wake, Curtois kuokoa mipira mingi ambayo ilikua ikielekezwa kwenye lango lake.

Katika dakika ya 54 ya mchezo, PSG kupitia Edinson Cavani ilifunga bao la kusawazisha. Hadi kipenga cha mwisho timu hizi mbili zilijikuta kikenda kwa kufungana bao 1-1.

Wakati huo huo, Bayern Munich ya Ujerumani, ikiwa ugenini, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ilimenyana na Shakhtar Donetsk na kutoka sare ya kutofungana.

Bayern Munich ilipata pigo kubwa baada ya mchezaji wake Xabi Alonso kuoneshwa kadi nyekundu na kuondolewa nje ya uwanja.

Leo Jumatano usiku, Real Madrid ya Hispania watakuwa wageni wa Schalke 04 ya Ujerumani katika mchezo mwingine wa klabu bingwa, huku Basel ya Uswis ikiikaribisha FC Porto ya Ureno.

Timu nyingine katika hatua hii ni Juventus ya Italia itakayopambana na Borussia Dortmund ya Ujerumani, Manchester City ya England itachuana na Barcelona ya Hispania.

Mechi zitakazochezwa usiku wa tarehe 24 Februari na tarehe 25 Februari ni Arsenal ya England itakuwa ikipimana nguvu na Monaco ya Ufaransa, huku Bayern Levkusen ya Ujerumani wakiwa wenyeji wa Atletico Madrid ya Hispania.

Mechi za hatua ya kumi na sita bora zitakamilika Machi 18, ambapo michezo miwili miwili itakuwa ikifanyika Jumanne na Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.