Pata taarifa kuu
SOKA-LIGI KUU YA UINGEREZA-LIVERPOOL

Steven Gerrard aamua kuachana na Liverpool

Nahodha wa klabu ya Liverpool nchini Uingereza, Steven Gerrard, ametangaza kuwa ataondoka katika klabu hiyo baada ya msimu huu kukamilika baadaye mwaka huu baada ya mkataba wake kukamilika.

Nahodha wa klabu ya Liverpool nchini Uingereza, Steven Gerrard.
Nahodha wa klabu ya Liverpool nchini Uingereza, Steven Gerrard. Liverpool FC
Matangazo ya kibiashara

Gerrard mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka tisa na kujiunga na kikosi cha wachezaji chipukizi.

Kwa kipindi hicho chote Gerrard ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Uingereza ameifungia Liverpool mabao 180 katika mechi 695 alizocheizea klabu yake.
Mchezaji huyo amesema huu umekuwa uamuzi mgumu sana kuufanya lakini analazimika kufanya hivyo, kwa kile anachokisema angependa kupata uzoefu katika sehemu nyingine.

Duru zinasema huenda Gerrard akaelekea nchini Marekani kucheza soka nchini humo, lakini amesisitiza kuwa hawezi kucheza nchini Uingereza na kukutana tena na klabu yake.

Atakumbukwa kuisaidia Liverpool kunyakua taji la klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2005, mataji mawili ya FA na pia kuisaidia klabu yake kushinda ligi kuu ya soka nchini Uingereza mara tatu .

Kocha Brendan Rodgers amesema ni vigumu kupata maneno ya kueleza namna Gerrard alivyo na umuhimu katika klabu hiyo ya Liverpool.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.