Kombe la dunia Brazil 2014
Kikubwa kitakachokumbukwa mwaka huu unaokamilika ni michuano ya soka ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Brazil kati ya tarehe 12 mwezi Juni hadi tarehe 13 mwezi Julai.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Timu ya taifa ya Ujerumani iliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Argetina bao 1 kwa 0 katika mchuano wa fainali. Ni kwa mara ya nne Ujerumani unatwaa kombe hilo katika historia yake.
Uholanzi iliibuka katika nafasi ya tatu huku, wenyeji Brazil wakiibuka wanne.
Mfungaji bora alikuwa ni James Rodriguez kutoka Colombia aliyefunga mabao sita, huku Lionel Messi akiibuka kuwa mchezaji bora.
Bara la Afrika liliwakilishwa na Algeria, Cameroon, Ghana, Cote d'Ivoire na Nigeria.
Nigeria na Algeria zilifika katika hatua ya kumi na sita bora.