Pata taarifa kuu
LIGI KUU UFARANSA-PSG-OM-Soka

Soka: PSG yatamba uwanjani dhidi ya Marseille

Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imeishinda Jumapili Novemba 9 klabu ya Marseeille mabao mawili kwa nunge, katika mchuano ambao ulikua ukisubiriwa na watu wengi katika ligi kuu ya Ufaransa.

Mshambuliaji wa PSG, Ezequiel Lavezzi, akipambana na mchezaji wa Marseille, Brice Dja DjéDjé.
Mshambuliaji wa PSG, Ezequiel Lavezzi, akipambana na mchezaji wa Marseille, Brice Dja DjéDjé. RFI / Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

PSG inachukua kwa sasa nafasi ya pili katika michuano ya ligi kuu ya Ufaransa, wakati ambapo Olympique de Marseille (OM) ikiwa bado inaongoza katika michuano hiyo, ikiwa mbele ya PSG kwa alama 1.

Paris Saint-Germain, ambayo imechezea nyumbani, ilitawala mpira mnamo dakika 10 za kipindi cha mwazo cha mchezo bila hata hivo kuliona lango la Marseille.

Bao la kwanza la PSG limewekwa wavuni katika dakika 38 za mchezo na mchezaji kutoka Brazil, Lucas Moura, baada ya kumsinda mbiyo beki wa Marseille Benjamin Mendy.

PSG ilitawala pia mpira katika kipindi cha pili cha mchezo, baada ya mshambuliaji machachari wa PSG, Zlatan Ibrahimovic, kuingia uwanjani. Mchezaji huyo alikosekana uwanjani tangu Septemba 21.

Bao la pili lilipachikwa na Cavani katika dakika ya 86, na kupelekea PSG kuongoza kwa mabao 2-0.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.