Pata taarifa kuu
ITALIA-Ligi kuu ya Italia

Italia: Utata waibuka baada ya Juve kuimenya AS Roma

Mabao ya klabu ya Juventus yaliyoingizwa wavuni kupitia mikwaju ya penalti yamezua utata, na kulaumu refari aliyochezesha mechi hiyo, na kudai kwamba kulikua na uonevu.

Mshambuliaji wa Juventus, Carlos Tevez, ambaye ni raia wa Argentina, ashindwa kuingiza wavuni mkwaju wa penalti, katika mchuano na AS Roma. Oktoba 5 mwaka 2014.
Mshambuliaji wa Juventus, Carlos Tevez, ambaye ni raia wa Argentina, ashindwa kuingiza wavuni mkwaju wa penalti, katika mchuano na AS Roma. Oktoba 5 mwaka 2014. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Juventus imeimenya AS Roma mabao 3-2, huku refari, Gianluca Rocchi, akinyooshewa kidolea cha lawama kwamba aliegemea upande mmoja alipokua akichezesha mechi hiyo.

Juventus imeingiza mabvao mawili kufuatia mikwaju ya penalti, huku AS Roma ikiingiza wavuni bao maja kupitia mkwaju wa penalti.

Bao la tatu la Juventus limeingizwa na Bonucci baada ya kupewa pasi nzuri na Gervinho, huku wachezaji wake wawili wakiwa wameotea.

Wakati huo huo kadi za manjano na wekundu zilitolea hovyo na refari. Meneja wa AS Roma, Rudi Garcia alifukuzwa nje ya uwanja baada ya kupinga penalti ya kwanza, huku kadi sita za manjano na mbili za wekundu zikipewa baadhi ya wachezaji kutoka timu hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.