Pata taarifa kuu

Mwanariadha wa Kenya Kimetto avunja rikodi ya dunia uya mbio za Marathon

Mwanariadha kutoka nchini Kenya Dennis Kimetto amevunja rekodi ya dunia ya mbio za Marathon baada ya kuibuka mshindi katika mbio za Berlin Marathon nchini Ujerumani leo Jumapili.

Dennis Kimetto mwanariadha kutoka nchini Kenya avunja rikodi ya dunia ya mbio za marathon
Dennis Kimetto mwanariadha kutoka nchini Kenya avunja rikodi ya dunia ya mbio za marathon REUTERS/Hannibal Hanschke
Matangazo ya kibiashara

Kimetto mwenye umri wa miaka 30 alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa mbili, dakika mbili na sekunde 57 na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Mkenya mwenzake Wilson Kipsang mwaka mmoja uliopita aliyemaliza mbio hizo kwa muda wa saa mbili, dakikatatu na sekunde 23.

Kimetto ambaye pia alishinda mbio za Tokyo Marathon na Bostin Marathon mwaka uliopita, amesema anajiskia vizuri baada ya kushinda leo, na kuvunja frekodi ya dunia kwa upande wa dunia.

Wanariadha wengine ambao pia wamewahi kuvunja rekodi ya dunia mjini Berlin ni Haile Gebreselasi kutoka Ethiopia mwaka 2008.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.