Pata taarifa kuu
BREZIL-Kombe la dunia

Mechi za kirafiki kwa kujiandalia Kombe la Dunia

Zikiwa zimesalia siku kumi na sita kuanza kwa kombe la dunia katika mchezo wa soka nchini Brazil tarehe 12 mwezi ujao, mataifa mbalimbali yanajiandaa kushirikia katika michuano hii mikubwa duniani.

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa "Les Bleus", Didier Deschamps, amemteua beki wa klabu ya Liverpool Mamadou Sakho nahodha wa kikosi cha leo.
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa "Les Bleus", Didier Deschamps, amemteua beki wa klabu ya Liverpool Mamadou Sakho nahodha wa kikosi cha leo. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa "Les Bleus" wakiwa mazoezini kwa maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia..
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa "Les Bleus" wakiwa mazoezini kwa maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia.. RFI/Pierre René-Worms

Leo usiku, katika uwanja wa Stade de France jijini Paris, timu ya taifa ya Ufaransa “Les Bleus” watamenyana na Norway katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki.

Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amemteua beki wa klabu ya Liverpool Mamadou Sakho nahodha wa kikosi cha leo.

Baada ya mchuano wa leo, Ufaransa pia itacheza na Jamaica na Paraquay.
Ufaransa itafungua mchuano wake wa kombe la dunia dhidi ya Honduras tarehe 15 mwezi ujao.

Timu ya taifa ya Ufaransa "Les Bleus" inawapa matumaini mashabiki wake kwamba itafanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia.
Timu ya taifa ya Ufaransa "Les Bleus" inawapa matumaini mashabiki wake kwamba itafanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia. RFI/Pierre René-Worms

Mbali na Honduras “Les Bleus” iko katika kundi moja na Swizerland, na Ecudor .
Katika michunao mingine ya kirafiki iliyochezwa jana usiku, Indobitbale Lions ya Cameroon iliifunga Macedonia mabao 2 kwa 0,

Maboa ya Cameroon yalitiwa kimyani na Pierre Webo katika dakika ya 52, Choupo Moting katika dakika ya 83.

Ubelgiji nayo ilifunga Luxembourg mabao 5 kwa 1, huku mchezaji matata wa klabu ya Everton Romelu Lukaku akifunga mabao 3 katika mchuano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.