Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Michezo

Manchester United yamtangaza Louis Van Gaal kuwa kocha wake mkuu, Giggs kuwa msaidizi wake

media Louis van Gaal, kocha wa timu ya taifa ya uholanzi aliyetangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Manchester United eurosport.com

Klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza imemtangaza kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo huku akimteua Ryan Giggs kama kocha msaidizi.

 

Vana Gaal mwenye umri wa miaka 62 hivi sasa ametia saini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha timu hiyo akichukua mikoba ya kocha David Moyes aliyetimuliwa baada ya kuwa na msimu mbaya kwenye timu hiyo.

Kufuatia uteuzi wake na yeye kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi inamaanisha kuwa hawezi kujiunga na klabu hiyo kwasasa mpaka pale michuano ya kombe la dunia nchini Brazil itakapokamilika.

Van Gaal amabye amekuwa na mafanikio makubwa wakati alipokuwa mwalimu vilabu vya Ajax, Barcelona, na Bayern Munich ambapo kwa nyakati tofauti alifanikiwa kupata mataji akiwa na timu hizo na sasa anakuwa kocha wa kwanza kutoka nje ya muungano wa nchi za Uingereza kama kocha mkuu wa Manchester United.

Kwenye taarifa yake, Louis Van Gaal amesema kuwa “Hii ni nafasi ya kipekee ambayo nimekuwa nikiisubiri kwa muda mrefu kufundisha klabu kubwa kama manchester United” anasema Van Gaal.

Kocha huyu ameongeza kuwa kufanya kazi na timu hiyo kubwa duniani na yenye mafanikio kunamfanya ajione moja kati ya makocha wenye bahati na mwenye kujisikia fahari kubwa.

Akinukuliwa na vyombo vya habari vya nchini mwake Van Gaal anasema “timu hii ina matarajio makubwa. Namimi nnamatarajio makubwa. Na kwa kwapamoja nnauhakika wa kuweka historia”.

Punde mara baada ya uteuzi wake, Van Gaal amemtangaza aliyekuwa kocha mchezaji wa timu hiyo, Ryan Giggs kama kocha wake msaidizi ambao watafanya kazi kwa mara ya kwanza msimu ujao.

Akizungumzia uteuzi wake, Giggs anasema kuwa amefurahishwa sana na anaona fahari ya kufanya kazi kwa pamoja na Louis Van Gaal.

Giggs anasema kuwa “Van Gaal ni kocha bora duniani na najua nitajifunza mengi kuhusu ufundishaji kutoka kwake na kuwa na ushirikiano nae wa karibu kwa kipindi chote atakachokuwa hapa”.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana