Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Japan

Imeshiriki mara 4, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 47 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Timu ya taifa ya Japan imekuwa ikishindwa kufikia ndoto zake kufika fainali za kombe hili na mara zote imekuwa ikipoteza mech zake tatu za awali. Hata hivyo mwaka 2002 kwenye fainali za Korea na Japan bado walishuhudia wakiondolewa mapema licha ya kuwa mwenyeji. Mwaka 2010 hata hivyo walifanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili na kukaribia hata hatua ya kumi na sita bora lakini wakashindwa kutimiza ndoto zao. 

Timu ya Taifa ya Japan
Timu ya Taifa ya Japan fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Japan iko kwenye kundi C ikijumuishwa na timu za taifa za Colombia, Ugiriki na Ivory Coast, wachambuzi wa mambo wanaona kuwa Japan kutokana na aina yao ya mchezo wananafasi ya kusonga mbele safari hii na hata kufika hatua ya kumi na sita bora.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Wachezaji kama Keisuke Honda anayekipiga na klabu ya CSKA ya Moscow ni miongoni mwa wachezaji tegemezi, wako pia wachezaji kama Shinji Kagawa, Shinji Okazaki, Yasuhito Endo na Atsuto Uchida ni kati ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuonesha uwezo wa kuisaidia timu yao kusonga mbele.

Benchi la Ufundi.

Timu ya taifa ya Japan inaongozwa na kocha mkuu, Alberto Zaccheroni.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na Kazuyoshi Miura, Shunsuke Nakamura na Hidetoshi Nakata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.