Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Mexico

Imeshiriki mara 14, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 19 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Timu ya taifa ya Mexico ni maarufu kama “El Tri”, ni timu yenye historia ya kipekee kwenye fainali za kombe la dunia, kwa mfano katika mashindano matano yaliyopita ya kombe hili, Mexico ilifanikiwa kufika kwenye hatua ya kumi na sita bora huku Argentina ikizima ndoto zake kwenye michuano ya mwaka 2006 Ujerumani na mwaka 2010 nchini Afrika Kusini. Ni mara mbili pekee Mexico ilifanikiwa kufika kwenye robo fainali yote ikiwa ilifanyika kwenye ardhi yake mwaka 1970 na 1986. 

Timu ya Taifa ya Mexico
Timu ya Taifa ya Mexico fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Mexico yenyewe iko kwenye kundi A la michuano ya kombe la Dunia la FIFA kwa mwaka huu ikujumuishwa pamoja na timu ya taifa ta Brazil, Croatia na Cameroon, hili bado no oja kati ya makundi magumu kwenye michuano ya mwaka huu.

Wachezaji wakuangaliwa.

Baada ya kutofanya vema kwenye michuano kadhaa na kubadilisha benchi lake la ufundi mara kwa mara haitakuwa kazi rahisi kwa vijana hawa kufanya vema mwaka huu nchini Brazil. Mexico inawategemea wachezaji wake kama Javier Chicharito Hernandez, Andres Guadado na Giovani dos Santos, pia inawategemea wachezaji kinda kama Oribe Peralta, Raul Jimenez na Carlos Pena.

Benchi la Ufundi.

Timu hii inaongozwa na kocha mkuu, Miguel Herrera.

Mafanikio kwenye kombe la dunia la FIFA.

Ilifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la FIFA la shirikisho mwaka 1999 na kuwa washindi, Kombe la dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2005 nchini Peru na kuwa washindi.

Wachezaji waliovuma.

Antonio Carbajal, Hugo Sanchez, Jorge Campos na Cuauhtemoc Blanco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.