Pata taarifa kuu
KENYA-RIADHA

Bendera ya Kenya yapeperushwa katika mbio za London Marathon

Bingwa wa dunia katika mbio za Marathon kwa upande wa wanaume Wilson kipsang kutoka nchini Kenya, aliwaongoza wenzake Stanley Biwwot na Edna Kiplagat na Florence Kiplagat kupeperusha bendera ya Kenya katika mbio za London Marathon zilizofanyika jana Jumapili.

Wilson Kipsang (kushoto) na Edna Kiplagat (kulia), wakipiga picha na rais wa kenya Uhuru Kenyatta mjini London London Aprili 13, 2014.
Wilson Kipsang (kushoto) na Edna Kiplagat (kulia), wakipiga picha na rais wa kenya Uhuru Kenyatta mjini London London Aprili 13, 2014. RS/EREUTEddie Keogh
Matangazo ya kibiashara

Wilson Kipsang a remporté akishinda kwa mara ya pili mbio za London marathon, avril 13, 2014.
Wilson Kipsang a remporté akishinda kwa mara ya pili mbio za London marathon, avril 13, 2014. REUTERS/Eddie Keogh

Kwa upande wa wanaume, Kipsang alimaliza mbio hizo za Kilimota 42 katika nafasi ya kwanza kwa muda wa saa mbili na dakika nne na seunde 29 na kuvunja rekodi ya mbio hizo iliyowekwa na mkenya mwenzake Emmanuel Mutai mwaka 2011 ya muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 40.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na mwenzake Stanley Biwwot aliyemaliza kwa muda wa saa 2 na dakika 55 huku mwithiopia Tsegaye Kebede aliyenyayakua taji hili mwaka uliopita akimaliza wa tatu kwa muda wa saa 2 na dakika sita.

Mwingereza Mo Farah aliyekuea anaangaliwa sana katika mbio hizo alimaliza wa nane kwa muda wa saa mbili na dakika nane.

Kwa upapnde wa akina dada, mkenya edna Kiplagat ameshinda mbio hizo kwa muda wa saa mbili na dakika 20 na sekunde 21 huku nafasi ya pili ikinyakuliwa na mkenya mwenzake Florence Kiplagat aliyemaliza kwa muda wa saa mbili, na dakika 20 na sekunde 24 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mwiethiopia Tirunesh Dibaba kwa saa mbili na dakika 20 na sekunde 35.

Mke wa rais wa Kenya , Magaret Kenyatta ambaye alishiriki mbio hizo kwa ajili ya kukusanya fedha za kuwasaidia wanawake, kupata matibabu ya afya ya uzazi pamoja na watoto alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa 7 dakika 5 na sekunde 28.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.